Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania, Athumani Mlinga (wa tatu kulia) akimtamza mwanafunzi wa shule ya kituo cha kulelea Watoto yatima cha Kiwalani, Janeth Lwanga (wa kwanza kushoto) akisoma mojawapo ya kitabu vilivyokabidhiwa kama msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kama vile madawati, meza, viti, vitanda, magodoro, na kompyuta vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Wakifuatilia tukio hilo ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kiwalani, Bw. Leornard Kingu Msusu (wa kwanza kulia), Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiwalani, Bi. Lucresia Francis Shayo (wa pili kulia) pamoja na Mwalimu wa kituoni hapo, Bi. Yustina Myovera (nyuma ya mwanafunzi).


Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bi Vivienne Penessis (katikati), na Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Athumani Mlinga (wa pili kulia) kutoka Vodacom Tanzania Plc, wakikabidhi baadhi ya msaada wa vitabu pamoja na vifaa vinginevyo vya shule kwa Mwasisi na Mwanzilishi wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Kiwalani, Mchungaji Elias Mwakalukwa (wa kwanza kushoto) na mwanafunzi wa shule ya kituoni hapo, Cecilia Teotimo (wa pili kushoto) wakati Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiwalani, Bi. Lucresia Francis Shayo (wa kwanza kulia) akishuhudia tukio hilo. Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kama vile vitabu, madawati, meza, viti, vitanda, magodoro, na kompyuta vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 ikiwa ni jitihada za kuisadia jamii mwishoni mwa wiki.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...