
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akitoa cheti kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Gs1 Tanzania Bi. Fatuma Kange wakati wa kufunga wiki Barcode kitaifa 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni, 19, 2023.
KATIKA kuhakikisha Wajasiriamali wanapenya kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya GS1 wamehamasisha wananchi kununua bidhaa zinazozalishwa nchini na nyenye msimbomilia ( Barcodes au QR code ).
Akizungumza wakati wa kufunga wiki Barcode kitaifa 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni, 19. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema kuwa 620 ni Mali ya Watanzania hivyo jamii imehamasishwa kununua mali ya Tanzania kwa 620.
"Tujisikie fahari kununua mali ya Tanzania yenye 620, ukinunua Mali ya Tanzania yenye 620 maana yake umesaidia nchi kupata mapato, pia pale unapoenda kutafuta Barcode kuna malipo unafanya hapo pia unachangia mapato ya Serikali." Amesema Mpogolo
Pia amesema kuwa Barcode ya Tanzania itapunguza maneno ya kashfa juu ya nchi kuwa inazalisha bidhaa zisizokuwa na ubora pia itapunguza bidhaa za nchi nyingine zinapoharibika na kusema ni bidhaa za Tanzania.
Akizungumzia umhimu wa Barcode amesema kuwa alama za Msimbomilia kwenye bidhaa za Tanzania Mpogolo amesema alama hizo zitasaidia Wafanyabiashara kupeleka bidhaa katika mataifa mbalimbali duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na vongozi wengine wakitembelea mabanda ya wajasiriamali wakati wa kufunga wiki Barcode kitaifa 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni, 19, 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akizungumza wakati wa kufunga wiki Barcode kitaifa 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni, 19, 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akitoa vyeti wakati wa kufunga wiki Barcode kitaifa 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni, 19, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...