Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakari Kunenge amezindua Jengo la Zahanati kwenye Kituo cha watoto yatima Kibaha Children Village Center kilichopo Mtaa wa Simbani Halmashauri ya Mji Kibaha chenye watoto 16 kinachoendeshwa na Mwenyekiti wa fursa Sawa kwa wote Mama Anna Mkapa.
Ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi 480 milioni kwa ufadhili wa Balozi wa Heshima wa Tanzania Ujerumani Mhe.Petra Hammelmann kupitia taasisi yake ya Paulchen Esperanza Foundation kwa kushirikiana na Werderhausen Foundation zote za nchini Ujerumani.
Akitoa taarifa kwa Mhe.Kunenge aliyefika kumwakilisha Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Angelah Kairuki,Mama Anna Mkapa amesema Zahanati hiyo itawahudumia wanafunzi na wakazi wa Mtaa wa Simbani zaidi ya 200 huku ikiwapunguzia adha ya kutembea zaidi ya Kilometa 20 walizotumia awali kufuata huduma za afya mahali pengine huku akitoa ombi Serikali kumwesha samani,dawa na watumishi ili kuanza kutoa huduma.
Mhe.Kunenge amempongeza Mama Anna Mkapa na bodi ya wadhamini ya EOTF kwa dhamira yao chanya ya kutoa huduma ya Afya kuunga Mkono Jitihada za Dr.Samia Suluhu Hassan,Rais wa Tanzania na kwamba Serikali pekee yake bila kuungwa Mkono na wadau haiwezi kutoa huduma maeneo yote kwa wakati.
Aidha,Mhe.Kunenge amekiri kuyafikisha maombi yote kwa Mhe.Waziri na ameahidi kuyatafutia ufumbuzi maombi yote yaliyopo ngazi ya Mkoa.
Hata hivyo Mhe.Kunenge ametoa rai kwa taasisi zote zisizo za kiserikali,sekta binafsi,wadau wa Maendeleo kuwekeza kwenye sekta ya Afya ili kuikwamua jamii kutoka kwenye wimbi la maradhi
Equal Opportunities For All Trust Fund (EOTF) ni taasis isiyo ya Kiserikali iliyoasisiwa 1997 ikiwa na dira ya kutoa fursa Sawa kwa jamii duni hasa kwa wanawake na Vijana kujikomboa kutoka kwenye wimbi la Maradhi,umasikini na Ujinga.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akiwa na mfadhili wa kituo hicho Petra Hammelmann ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi yake ya Esperanza Foundation
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...