NA VERO IGNATUS,ARUSHA

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kuzalisha vazi la batiki ili kuepuka kuwa tegemezi kiuchumi

Ameyasema hayo leo julai 8,2023 Jijini Arusha katika maadhimisho ya kwanza baada ya uzinduzi, kwamba vyema wajasiriyamali wakashikamana kwani Arusha ndiyo kituo cha batiki Tanzania, na ili waweze kufanikiwa lazima wajikite kwenye ubora na viwango pamoja na mishono bora yenye kuvutia

"Niwatake Sido, Ofisi ya maendeleo ya mkoa, mkemia mkuu pamoja na ROIJOIK tutengeneze programu maalum ya kufanya kila mtu ajue kuwa unaoozungimzia batiki nenda Arusha, ili tusaidiane nasema hii ajenda tunaibeba kama mkoa,Tupate na vijana wabunifu washone watu watamani kwasababu soko ni la ushindani na ubora wa bidhaa yako" alisisitiza Mongella

Akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi Roijok Progress Centre, Rose Urio na mwanzilishi wa batiki Project Tanzania Rose amesema kuwa mradi huo ulifunguliwa julai 2022 ambapo waliiomba serikali katika sherehe za kitaifa kuvaliwe Batiki

Aidha mwaka huu 2023 katika sherehe za kitaifa wanawake nchi nzima walivaa batiki chini ya mradi wa batiki project Tanzania ambapo kupitia vazi la batiki wanaenda kukuza utalii,kujenga umoja na kuitambulisha nchi katika ngazi ya Kimataifa.

"Changamoto kubwa tukigoikuta katika masoko ya Kimataifa ni namna ya utengenezaji wetu wa batiki, kwa 99% inatengenezwa kwa kutumia kuni na mkaa hivyo kuharibu mazingira na kuleta athari kubwa katika dunia, kwakuliona hilo novemba 2022 tulizindua sifastove kwajili ya uzalishaji

Pamoja na hayo pia waliweza kutambua kuwa hakuna batiki inayoitambulisha Tanzania ndani na nje hivyo wakaamua kubuni batiki yenye rangi ya tanzanite kutokana na kuwa nakito cha thamani na yanapatikana nchini katika mkoa wa Manyara.

"Hiyo ndiyo imekuwa sababu kubwa ya kuwa na Samia Tanzanite Print tunakwenda kuiweka katika kilele cha mlima na kuiambia dunia kwamba sisi Tanzania tuna print yetu "alisema

Mradi wa batiki unafaida kubwa na tumekuwa tukiwahimiza vijana kujikita humo ili kujikwamua kiuchumi , kwamfano unapotengeneza batiki pic 100,000 faida yake mil200 ,inamaana kikundi chenye vijana 10 wakapata hiyo pesa kwa mwaka hiyo ni faida kubwa na hakuna mradi wa uwezeshaji mdogo mdogo unaoweza kupata faida kubwa namna hiyo

Bi Rose amesema kuwa Kwa kupitia Mradi huo wa uzalishaji wa Batiki vijana watakuza vipato vyao lakini pia wataona thamani ya Elimu yao,huku baada ya batiki kupata viwango vinavyohitajika itasaidia kujiuza na kupata masoko mengine mengi makubwa.

Rose amesema kuwa maono yao ni kuona Batiki zikiwasaidia akinamama kiuchumi, ikiongeza pato la Taifa lakini pia tunapoongelea Uchumi na Batiki iwepo.

Mara baada ya uzinduzi wa batiki kufanyika Julai 8, 2022, wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Batiki Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya Kibiashara ya 46 jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la Kuitangaza Batiki ndani na Nje ya Nchi, mwaka 2023 siku ya wanawake zilivalia pisi mil 4 ,huku Jiji la Arusha zikivaliwa pisi 200,000

Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongella akikata utepe ishara ya Onyesho la kwanza baada ya kuzindua siku ya Batiki Tanzania kulia kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi Roijok Progress Centre, Rose Urio na Muasisi wa Batiki project Tanzania uliyozaa uvaaji wa batiki.
Wanawake wakiwa na katika picha ya pamoja na. Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella mara baada ya Onyesho la kwanza la Vazi la batiki, baada ya Uzinduliwa uliofanyika mwaka jana julai 8 2022 Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Taasisi Roijok Progress Centre, Rose Urio na Muasisi wa Batiki project Tanzania uliyozaa uvaaji wa batiki. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...