NA. VERO IGNATUS,ARUSHA
Ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya siku ya kupiga mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika inayoadhimishwa ambayo yameambatana miaka 20 ya utekelezaji wa maazimio Barani Afrika ya kupambana na Rushwa ambapo yatajumuisha washiriki 700 kutoka katika sekta mbalimbali nchini na nje ya nchi
Akizungumza kwa niaba ya Rais Mwinyi, jijini Arusha katika uzinduzi wa maadhimisho hayo ya siku tatu yaliyoanza julai 9 hadi 11,2023,Makamu wa wapili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman alisema ni vyema wanachi wakatumia maadhimisho hayo katika kujitathmini pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vitendo hivyo
Amesema kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza wawakilishi Zanzibar,Dk Hassan ali Mwinyi amewataka wananchi na viongozi mbalombali kutumia maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa barani Afrika kujitathmini juu ya hatua walizochukua katika kupambana na vitendo vya rushwa katika maeneo yao.
"Kila nchi kwa ujumla ni jukumu lao kujitathmini ni hatua gani wamechukua dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa katika sekata mbalimbali na katika utendaji kwa kushikamana na kuwa chachu muhimu ya kuongeza kasi katika utendaji"alisema
Tanzaia ilikuwa nchi ya mwanzoni kusaini mkataba huo wa kuzuia na kupoambana na rushwa 2003 nchini Malawi hivyo 2023 Nchi imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo.
Mhe.Abdulla amesema kuwa rushwa ni adui wa hali na kikwazo cha maendeleo yeyote duniani hibyo ni jukumu la Kila mmoja kuhakikisha anapambana ili kuleta maendeleo.
Amewawataka wananchi kutumia maadhimisho hayo yenye mafunzo kutoa taarifa mbalimbali za vitendo vya rushwa vinavyoendelea, kwani mapambano dhidi ya rushwa yanamuhusu kila mmoja.Serikali yahamasisha wananchi kutumia fursa ya maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa katika kubadilishana uzoefu wa kupambana na vitendo hivyo nchini na barani Afrika kwa lengo la kusaidia jamii upatikanaji wa haki bila kutoa rushwa.
"Maadhimisho haya ya siku 3 yameandaliwa kwa ajili yetu sisi wahusika kwani ni muda muhafaka wa kujipanga zaidi katika kupambana na rushwa hivy kila mwanachi kutoka nchi za Afrika na sio Taasisi za rushwa pekekee,"alisema Makamu wa pili wa Zanzibar.
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,George Simbachawene alisema Tanzania iko tayari kushirikiana na mataifa mengine katika mapambano dhidi ya rushwa.
Aidha Simbachawene amesisitiza na kutaka jamii itambue Rushwa siyo rafiki katika kuleta maendeleo hivyo Maadhimisho haya yatawaleta pamoja na sambamba na Mamlaka kupeana uzoefu namna gani wataweza kutokomeza rushwa barani Afrika.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, CP.Salum Hamduni alisema Julai 11 kila mwaka ni siku iliyotengwa na Umoja wa Afrika kuadhimisha mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika ambapo ni maadhimio ya mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika Adis ababa nchini Ethiopia julai 3 hadi 4,2017.
Hamduni amesema siku hii inatokana na maazimio ya mkutano wa 29 wawakuu wa Umoja wa nchi za Afrika uliofanyika julai 3-4 ,2017 AdisAbaba Ethiopia
"Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ni mafanikio baada ya miaka 20 wa utekelezaji wa mkataba wa Umoja wa Afrika wa kuzuia kupambana na rushwa na Matarajio yake,"alisema Mkurugenzi Hamduni.
Mkurugenzi Hamduni amesema kuwa maadhimisho ya mwaka 2023 yataambana na shughuli mbalimbali ikiwemo maonyesho ya asasi za kiraia ambapo yamewekwa mahususi katika kutoa elimu ya masuala ya rushwa kwa wananchi.
Mkurugenzi huyo amesema Julai 10 kutakuwa na kongamano la wadau litakalofunguliwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,George Simbachawene ambapo litahusisha majadiliano ya mada mbalimbali ikiwemo uzoefu wa Taasisi za kupambana n rushwa barani Afrika kwa miaka 20 iliyopita tangu kusainiwa kwa mkataba wa umoja wa Afrika wa kupambana na rushwa.
Amesema mada nyingine ni pamoja na uzoefu katika urejeshwaji mali zilizopatokana kwa njia ya rushwa na mazalia yake,Mchango wa Asasi za kiraia katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa,mchango wa vijana katika mapambano dhidi ya rushwa katika ulimwengu wa Kidigitali.
Pia amesema mada nyingine ni matumaini baada ya miaka 20 ya utekelezaji wa mkataba wa umoja wa Afrika katika mapambano dhidi ya rushwa,athari za rushwa katika sekta ya elimu kupata uzoefu katika nchi wananchama, Utafiti katika kijikita katika ushahidi kuhusiana na mikakati dhidi ya kupambana na rushwa pamoja na tathmini ya mchango wa Taasisi za kimataifa na wadau wa maendeleo katika utekelezaji wa mkataba wa Umoja wa Afrika katika kupambana na rushwa.
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Arusha wamesema wanapata changamoto ya kukabiliana na vitendo vya rushwa kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya rushwa hali inayopelekea jamii kuamini rushwa ni haki yao.
Makamu wa wapili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman akizungumza katika Ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya siku ya kupiga mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika inayoadhimishwa ambayo yameambatana miaka 20 ya utekelezaji wa maazimio Barani Afrika ya kupambana na Rushwa ambapo huadhimishwa kila julai 11
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,George Simbachawene: Tanzania iko tayari kushirikiana na mataifa mengine kutokomeza rushwa
Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, CP.Salum Hamduni: Julai 11 kila mwaka ni siku iliyotengwa na Umoja wa Afrika kuadhimisha mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika.
Baadhi ya Wageni walioshiriki katika Ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya siku ya kupiga mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika inayoadhimishwa kila julai 11 kila mwaka.
Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, CP.Salum Hamduni akiteta jambo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa
Baadhi ya Wageni walioshiriki katika Ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya siku ya kupiga mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika inayoadhimishwa kila julai 11 kila mwaka.
Ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika yanayofanyika leo jijini Arusha Bendi ya Polisi ikiongoza matembezi ya kam 2.5 kwaajili ya maadhimisho hayo
Makamu wa wapili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman akiwasili katika Kituo cha kimataifa cha mikutano AICC kwaajili ya Ufunguzi wa mkutano wa Maadhimisho ya siku ya kupiga mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...