Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na Taasisi ya Benjamini Mkapa kuanzia mpango wa kutoa ufadhili wa masoso (scholaships) kwa wanafuzi wa taaluma ya ukunga nchini ili kuunga mkono juhudi za kupambana na changamoto za vifo vinavyotokana na uzazi kwa akina mama.

Kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia wakina mama wajawazito, jambo ambalo hupekea kutokea kwa vifo vingi vinavyoweza kuepukika.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2020, karibu asilimia 95% ya vifo vya akina mama wajawazito vilitokea katika nchi zinazoendelea huku idadi ya vifo hivyo kwa Tanzania ikiwa juu. Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya afya, kuongeza watumishi wenye ujuzi na nyinginezo.

Ushirikiano kati ya benki ya NBC na Taasisi ya Benjamini Mkapa ni wito wa wadau kuungana katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hili. Kupitia ushirikiano huu, NBC itatoa ufadhili wa masomo kwa wakunga na hivyo kuboresha huduma kwa wajawazito lengo likiwa ni kupunguza vifo vinavyoepukika.

Akiongea wakati wa hafla ya utiaji sahihi, Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi alisema benki ya NBC inayofuraha kutoa mchango wake katika kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

“Tukiwa kama benki inayothamini ustawi wa jamii tunajivunia kutoa mchango wetu kusaidia maendeleo ya jamii ambayo tunaihudumia. Tunafahamu umuhimu na uharaka wa kushughulikia suala la vifo vinavyotokana na uzazi hapa nchini na tunaamini uwekezaji kwenye elimu na mafunzo kwa wakunga wetu kutasaidia sana kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika. Ni furaha kwetu kutoa sehemu ya kiasi kinachopatikana kutokana na uchangishaji fedha wetu wa kila mwaka kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon na kuzielekeza kwenye utatuzi wa chagamoto hii,” alisema.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt. Ellen Mkondya aliishukuru benki ya NBC na kuwataka wadau wengine kufuata mfano wa benki hiyo ili kuongeza nguvu katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.

“Tunayofuraha kushirikiana na benki ya NBC katika lengo letu kuu la kupambana na vifo vya wajawazito hapa nchini. Ufadhili wa masomo unaotolewa na benki ya NBC utasaidia kuboresha ujuzi wa wakunga wetu na hivyo kuboresha huduma za uzazi salama,,” alisema

Kupitia ushirikiano huo wa miaka miwili, NBC itatoa kiasi cha shilingi milioni mia mbili (200m) ambazo zitatumika kusomesha wakunga 100 katika kipindi husika na hivyo kusaidia kuongeza nguvu kazi yenye ujuzi katika kuwahudia akina mama wajawazito.

Benki ya NBC na taasisi ya Benjamini Mkapa zinaamini kuwa uwekezaji katika elimu na mafunzo kwa wakunga ni hatua muhimu sana katika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo endelevu namba 3 ambalo linalenga kusaidia ustawi kwa wote ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (aliyekaa kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt. Ellen Mkondya (aliyekaa kushoto) wakitia  saini makataba wa  makubaliano baina ya taasisi hizo mbili ambapo Benki ya NBC itatoa kaisi cha shilingi milioni mia mbili (200m) kusomesha wakunga 100 katika kpindi cha miaka 2 ikiwa ni mchango wake katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt. Ellen Mkondya wakionyesha mkataba waliosaini kusaidia mapambano dhidi ya vifo vinavyotokana na uzazi hapa nchini. Kupitia mkataba huo Benki ya NBC itatoa kaisi cha shilingi milioni mia mbili (200m) kusomesha wakunga 100 katika kpindi cha miaka 2 ikiwa ni mchango wake katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (kulia) wakipeana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt. Ellen Mkondya muda mfupi baada ya taasisi hizo mbili kusaini mkataba wa kusaidia afya ya akina mama wajawazito. Kupitia mkataba huo Benki ya NBC itatoa kaisi cha shilingi milioni mia mbili (200m) kusomesha wakunga 100 katika kpindi cha miaka 2 ikiwa ni mchango wake katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt. Ellen Mkondya akiwa anatia sahihi katika bango la ushiriki wa mbio za NBC Dodoma Marathon muda mfupi baada ya taasisi hizo mbili kutiliana sahihi mkataba wa kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi. Anayetizama kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (wanne kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt. Ellen Mkondya (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hizo mbili muda mfupi baada ya muda mfupi baada ya  kusaini mkataba wa kusaidia afya ya akina mama wajawazito. Kupitia mkataba huo Benki ya NBC itatoa kaisi cha shilingi milioni mia mbili (200m) kusomesha wakunga 100 katika kpindi cha miaka 2 ikiwa ni mchango wake katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...