RC Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Holmes Matinyi ilani ya CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Holmes Matinyi akisaini hati ya kiapo baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Holmes Matinyi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo asubuhi Julai 4 2023 katika hafla ya uapisho iliyofanyika kwenye Ukumbini wa Mikutano ofisini kwa RC.

Na Khadija Kalili Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila leo Julai 4 2023 asubuhi amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temek Mheshimiwa Mobhare Holmes Matinyi .

Uapisho huo ni kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hafla ya Uapisho huo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkoa huo Ilala Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Sekretarieti na Wilaya za Mkoa huo wakiongozwa na

Katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

RC Chalamila memtakia majukumu mema DC Matinyi katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Temeke huku akitoa rai kwa Viongozi wa Manispaa na Wilaya kumpa ushirikiano kiongozi huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...