Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV- Mbeya

KATIBU  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo  amewasili katika  Uwanja wa Ndege wa Songwe jijini Mbeya, tayari kwa kufanya mkutano  mkubwa wa hadhara utakaofanyikaUwanja wa Luanda jijini humo.

Chongolo akiwa uwanja wa ndege amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wa mikoa jirani pamoja na  Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.

Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Chongolo ataelezea hatua kwa hatua  usahihi wa makubaliano ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa viwango vya hali ya juu tofauti na ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa ratiba ,mkutano huo utahudhuriwa pia na baadhi ya wananchi kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...