Na Said Mwishehe, Michuzi TV

TAASISI ya Mtetezi wa Mama imewakutanisha wananchi wa makundi mbalimbali jijini Dar es  Salaam na kufanya maandamano yenye lengo la kuhamasisha na kutambua juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia Watanzania wote.

Maandamano hayo yamefanyika leo Julai 15,2023 na kumalizikia katika Viwanja vya Leadersa jijini Dar es Salaam huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akitumia nafasi hiyo kuipongeza taasisi hiyo sambamba na kuhamasisha wananchi wote kuungana na Rais Samia katika kuleta maendeleo.

Akizungumza zaidi Mtemvu amesema Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa na nzuri ya kuleta maendeleo, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kwa nafasi yake kumuunga mkono ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kupata maendeleo.

“Tuna kila sababu ya kumuunga mkono Rais Samia ili aweze kufanikisha malengo yake ya kuendelea kutuletea maendeleo na kujenga uchumi imara badala ya kupinga kila jambo lenye mafanikio.”

Amesema Taasisi ya Mtetezi wa Mama imefanikiwa kueleza mambo makubwa ambayo yanafanywa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Dk.Samia hivyo watanzania nao wanawajibu wa kuunga mkono jitihada zake.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Taaisisi ya Mtetezi wa Mama Neema Karume, amesema kuwa baada ya utambulisho wa taasisi yao ambapo imeshirikisha mikoa 10 ya kueleza makubwa ya Rais anayofanya wataendelea kuelezea mazuri yanayifanywa na Rais katika maeneo mbalimbali nchini.

Pamoja na mambo mengine Karume amesema kuwa Rais Samia ameonesha upendo kwa Watanzania wote na amekuwa mwenye kusikiliza makundi yote bila kujali itikadi za kisiasa na ndio maana baada ya kuingia madarakani amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vyote vya kisiasa , lengo kuu ni kuwaunganisha Watanzania.

“Tunampenda sana Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan , hachagui yuko kwa ajili ya wananchi wote na ndio maana aliamua kukutana na viongozi wa vyama vyote na kuzungumza nao ili kutafuta maridhiano katika masuala mbalimbali.”

 Pia amesema Rais Samia ameendelea kuboresha sekta mbalimbali nchini kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu za kijamii huku akitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa jitihada zake katika kuboresha sekta ya elimu sambamba na utoaji elimu bure kwa watoto wa kitanzania.

“Mama kwenye sekta ya elimu ameweza na ameupiga mwingi kwasababu sasa hivi hakuna mzazi au mlezi anayeweza kuwa na kisingizio cha kukosa ada ya watoto wa shule.Rais wetu amehakikisha watoto wote wanapata elimu bure ili kutimiza ndoto zake, hili ni jambo ambalo limetuvutia sana na tutaendelea kumuunga mkono.”

Kuhusu huduma za afya, miundombinu,maji na umeme, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia imeendelea kuboresha sekta zote muhimu katika jamii akitoleo mfano wa nishati ya umeme na maji ambavyo vimepewa kipaumbele.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...