Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amelitaka Jeshi la Jadi Sungusungu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi badala ya kugeuka kuwa wahalifu kwa kuwatendea ukatili watuhumiwa wa matukio mbalimbali pindi wanapowakamata.
Mhe. Samizi ametoa agizo hilo leo Jumamosi Julai 1,2023 wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga Bila Uhalifu inawezekana iliyofanyika katika kata ya Ndala na Masekelo Manispaa ya Shinyanga ambayo imeanzishwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa uratibu wa Mwandishi wa Habari na Mshereheshaji Amos John maarufu MC Mzungu Mweusi.
“Serikali inatambua uwepo wa Jeshi la Jadi Sungusungu na tumekuwa tukishirikiana kutokomeza vitendo vya uhalifu katika jamii. Sungusungu hakikisheni mnasimamia sheria, kanuni na taratibu mlizojiwekea pamoja na za nchi”,amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
“Katika kata 43 za wilaya ya Shinyanga tuna majeshi ya sungusungu. Wafikisheni polisi wahalifu badala ya kujichukulia sheria mkononi. Haifurahishi na inatia hasira kuona baadhi ya sungusungu wanageuka wahalifu kwa kujichukulia sheria mkononi kuwafanyia ukatili watuhumiwa wa vitendo vya uhalifu”,ameongeza Samizi.
Katika hatua nyingine, Samizi amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo MC Mzungu Mweusi kuanzisha kampeni hiyo ya Kataa Uhalifu Shinyanga Bila uhalifu inawezekana hali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhalifu katika jamii.
“Ni jukumu la kila mmoja wetu kutoa taarifa pale anapobaini kuna viashiria vya uhalifu au uhalifu. Tuchukue hatua kuzuia uhalifu, tuache tabia za hovyo tunazoziita uhalifu”,amesema Samizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema wamepeleka Kampeni hiyo katika kata za Ndala na Masekelo kutokana na kwamba katika maeneo hayo bado kuna vitendo vya uhalifu ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya (bangi), ubakaji na wizi.
Aidha amesema Kampeni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa mkoani Shinyanga kwani vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji, ulawiti, ubakaji na ukabaji yamepungua hivyo kuwaomba wananchi kuendelea kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu.
Naye Kamanda wa Jeshi la Jadi la Sungusungu Manispaa ya Shinyanga John Kadama amesema jeshi hilo linaendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii.
Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo imeenda sanjari na Bonanza la Michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake ambapo pia kumefanyika zoezi la uchangiaji damu salama na utoaji elimu mbalimbali.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023. Picha na Kadama Malunde -Malunde 1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023.

Mratibu wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana, Amos John maarufu MC Mzungu Mweusi akizungumza wakati wa kampeni hiyo katika kata ya Ndala na Masekelo Manispaa ya Shinyanga

Kamanda wa Jeshi la Jadi la Sungusungu Manispaa ya Shinyanga John Kadama

Mchungaji Kiongozi katika Kanisa la Anglikana Ndala, Kasisi Sewando akizungumza wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023.

Diwani wa kata ya Masekelo Mhe. Peter Koliba akizungumza

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga wakitoa elimu ya namna ya kupambana na majanga ya moto wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga akionesha namna ya kuzima moto wakati wa Kampeni ya Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana katika kata ya Ndala na Masekelo leo Jumamosi Julai 1,2023.

Mchezo wa mpira wa miguu kati ya Ndala Combine na Masekelo Combine ukiendelea ambapo Masekelo waliibuka washindi kwa mikwaju ya penalti 5-3

Mchezo wa mpira wa miguu kati ya Ndala Combine na Masekelo Combine ukiendelea

Meza kuu wakifuatilia Mchezo wa mpira wa miguu kati ya Ndala Combine na Masekelo Combine

Polisi jamii kata ya Masekelo Yasinta akishangilia na wachezaji wa mpira wa miguu Masekelo Combine baada ya kuibuka washindi

Mbio za baiskeli kundi la wanawake zikiendelea ambapo mshindi wa kwanza ni Kipepeo Futi mbili akifuatiwa na Temineta

Mbio za baiskeli kundi la wanawake zikiendelea ambapo mshindi wa kwanza ni Kipepeo Futi mbili akifuatiwa na Temineta

Mbio za baiskeli kundi la wanaume zikiendelea ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Malaika Leonard akifuatiwa na Kashinje Kapemba na Konda Ishudu

Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Viongozi wa Jeshi la Sungusungu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Burudani ikiendelea

Burudani ikiendelea

Mwakilishi wa Mashabiki wa Yanga akipokea zawadi ya pesa baada ya mashabiki wa Simba na Yanga kucheza mpira wa miguu na mashabiki wa Simba kuibuka washindi

Mwakilishi wa mashabiki wa timu ya Simba akipokea zawadi ya mpira baada ya kuwashinda mashabiki wa Yanga

Mwakilishi wa Timu ya mpira wa miguu Masekelo Combine akipokea zawadi ya pesa na kombe

Mwakilishi wa Timu ya mpira wa miguu Masekelo Combine akipokea zawadi ya pesa na kombe

Mshindi wa Pili mbio za baiskeli kundi la wanawake,Temineta akipokea zawadi ya pesa

Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kundi la wanawake,Kipepeo Futi Mbili akipokea zawadi ya pesa

Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kundi la wanaume Malaika Leonard akipokea zawadi ya pesa

Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...