Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania (GST) imetoa toleo jipya la kitabu kinachoonesha madini yanayopatikana nchini Tanzania kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata hadi Kijiji.

Akizungumza katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama sabasaba, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba amesema kuwa toleo hili la tano limetoka mwaka huu wa 2023 likiwa limebeba taarifa nyingi zinazoonesha madini yanayopatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Dkt. Budeba aliongeza kuwa tofauti na toleo ya nne, toleo jipya ambalo ni la tano limesheheni taarifa nyingi zaidi na lina ramani ya kila mkoa inayoonesha jiolojia na madini yapatikanayo katika mkoa husika.

Dkt.Budeba alifafanua kuwa toleo husuka linategemewa kuendelea kuongeza uelewa wa wananchi na wadau wengine juu ya jiolojia na madini yanayopatikana katika maeneo yao na hivyo kuchochea uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Kupitia msimu huu wa sabasaba, GST imeendele a kutoa elimu kwa wananchi hasa wachimbaji wa madini juu ya umuhimu wa kutumia taarifa zinazotokana na tafiti za madini zinazofanywa na GSTili kuongeza tija katika shughuli zao.

Sambamba na utafiti wa madini , GST pia ina maabara ya kisasa inayotoa huduma za uchunguzi wa sampuli za miamba, madini, udongo na maji. Aidha, GST inajukumu la kuratibu majanga ya asili ya jiolojia kama matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkano na maporomoko ya udongo na kutoa ushauri wa kitaalam juu namna bora ya kupunguza athari zake.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...