MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema Rais Dk.Samia Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kuleta maendeleo kwa Watanzania katika kipindi kifupi cha uongozi.
Hivyo kinachopaswa kufanywa na kila mmoja ni kumuunga mkono, kumpa moyo na kuthamini yale anayofanya.
"Rais Samia ameongoza kwa miaka miwili, kama alivyosema Waziri wa Maliasili na Utali Mohamed Mchengerwa, haya ambayo mbunge anayasema yanafanyika katika kila jimbo nchini, kuna shughuli nyingi zinaendelea na Rais wetu si mtu wa kujitukuza, sio mtu wa kujisifia, yeye ni mtu wa vitendo
"Kila mahali katika nchi hii kuna kazi zinafanyika, miundombinu ya barabara, maji, hospitali, ujenzi wa shule na kwa mara ya kwanza wazazi hawajaambiwa wachange kujenga shule na kununua madawati, katika historia ya nchi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili zaidi ya madarasa 20,000 yamejengwa," alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...