Vivo Energy Tanzania imehitimisha msimu wa pili wa promosheni yake ya kitaifa ya “Jaza Ushinde Tena na Engen”. Promosheni hiyo iliwapa wateja fursa ya kuingia kwenye droo ya bahati nasibu kila mara wanapojaza mafuta ya kiasi cha TZS12,000 kwenye pikipiki na bajaji, TZS60,000 kwenye magari madogo, na TZS120,000 kwenye mabasi na malori.

Zawadi zilizokuwa zikishindaniwa ni pamoja na, vocha za chakula zenye thamani ya TZS100,000 na vocha za manunuzi zenye thamani ya TZS 100,000 kwenye maduka ya Engen, simu janja, friji, TV na Bodaboda kama zawadi kuu.

Michael Kida na washindi wengine Finias Boniface na Hatibu Kusaga wa mikoani ambao bado hawajakabidhiwa zawadi zao, Kida aliondoka na ushindi wa pikipiki mpya kabisa. Gaston Beatus, Fikiri Mtimbuka na Francis David waliondoka na runinga janja za inchi 43, na Edward Mria, Alphan Hassan na Said Mambongo walibeba friji mpya pamoja na washindi wengine wa simu janja, vocha za chakula na vocha za ununuzi. Hii inafanya jumla ya washindi 18 wakati wa kampeni hii.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Vivo Energy Tanzania, Khady Sene, aliwashukuru wateja kwa kuchagua vituo vya Engen na kuahidi kwamba kampuni hii itaendelea kutoa bidhaa na huduma zilizobora sambamba na kueneza huduma kote nchini, mpaka sasa tuna vituo 41 na tutaendelea kuviongeza kuhakikisha kwamba watanzania wengi wanafurahia huduma zetu.


Mmoja wa washindi watatu wa pikipiki, Michael Kida alisema, 'Napenda kuwahimiza wateja ambao wana shaka na mashindano, kuchukua nafasi kwa sababu mambo mazuri hutokea - siku zote nilitaka kuwa na chanzo cha ziada cha mapato na leo nimekipata, shukrani kwa Engen, kwa kuniwezesha kufanya hili.'

Grace Kijo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vivo Energy Tanzania alisema kuwa kampeni ya “Jaza Ushinde Tena na Engen” ni mwanzo tu wa kampeni nyingi za kusisimua tulizoziandaa, hivyo wateja wetu wanapaswa kutarajia zaidi kila wakati kwa sababu kwetu sisi wewe ni namba moja, kila mara huwa tunatengeneza bidhaa tofauti tofauti kwa maslahi ya mteja. 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vivo Energy Tanzania, Khady Sene (kulia) akimkabidhi funguo  mshindi wa promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen, Michael Kida mkazi wa Kipinguni Gongolamboto aliyejishindia pikipiki mpya baada ya  kushiriki kujaza mafuta kwenye vituo vya Engen na kuingia kwenye droo hiyo, makabidhiano hayo yalifanyika Kipunguni jijini Dar es salaam. Wengine wapili kulia  Msimamizi wa Kituo cha Kipunguni Muslim Baruani na kushoto ni Meneja wa Mauzo ya Rejareja Vivo Energy Tanzania, Adams Ouedrago.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vivo Energy Tanzania, Khady Sene (watatu kulia) akimkabidhi Runinga mshindi wa promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen, Gaston Beatus mkazi wa Bunju jijini Dar es salaam aliyejishindia  zawadi hiyo baada ya  kushiriki kujaza mafuta kwenye vituo vya Engen na kuingia kwenye droo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vivo Energy Tanzania, Khady Sene (watatu kulia) akimkabidhi Friji na shopping vocha mshindi wa promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen, Edward Peter Mria mkazi wa Tabata Kinyerezi jijini Dar es salaam aliyejishindia zawadi hiyo baada ya  kushiriki kujaza mafuta kwenye vituo vya Engen na kuingia kwenye droo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vivo Energy Tanzania, Grace Kijo akizungumza wakati hafla ya promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...