Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewataka viongozi wa CCM Wilaya ya Kibiti mkoni Pwani kuimarisha umoja na mshikamano kwa kuwa ndio siri ya maendeleo.
Kinana ameyasema hayo leo Julai 15, 2025 alipozungumza na viongozi mbalimbali katika kikao cha ndani baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi Mpya ya CCM Wilaya ya Kibiti.
Amesema mafanikio yanayoendelea kuonekana katika wilaya hiyo hususani kwa Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2020-2025) ni matokeo ya umoja, mshikamano na ushirikiano, hivyo ni vyema waendelee kushikama kufanikisha kupatikana kwa mafanikio makubwa zaidi.
Aidha Ndg Kinana amewapongeza Viongozi na Wanachama kwa Ushindi wa Kishindo kufuatia uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Mahege ambapo mgombea wa CCM Ndg Hamada Juma Hingi aliibuka mshindi kwa asilimia 85.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...