Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imepokea treni ya Kitalii Kampuni ya ROVOS yenye Watalii 60 kutoka nchini Afrika Kusini.

Treni hiyo ilianza safari yake mwezi Juni 30, 2023 na imepita katika nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na kuhitimisha nchini Tanzania.

Afisa Utalii Mkuu Bi. Alistidia Karaze amesema kuwa Bodi ya Utalii Tanzania Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea Watalii 60 waliotoka Mataifa ya, Denmark, Canada, Australia, Malaysia, Marekani na Afrika Kusini.

"Watalii hawa wamekuja na treni ya ROVOS  alionza safari kutoka Afrika Kusini, wakiwa nchini watapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar" amesema Karaze

Ameongeza kuwa tukio hilo ni kutokana na juhidi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan Suluhu kupitia filamu ya " The Royal Tour" kutangaza utalii duniani.

Mtalii Andrew Saimon  kutoka Marekani amefurahishwa na mapokezi makubwa kutoka Tanzania na kuwapongeza watanzania Kwa kuwa watu wakarimu na wenye upendo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...