Na Rahma Khamis Maelezo              21/7/2023

 

Wakufunzi wa Chuo cha  Mafunzo Zanzibar wametakiwa kuchukua  juhudi za makukusudi ili kuhakikisha  Sheria  ya Chuo inakuwepo Chuoni hapo ili wanafunzi ,Maafisa  na wananchi  waweze kuifahamu.

Akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Magereza juu ya kuwaongoza wananfunzi wanawake  huko Ofisini kwao Magreza Mhadhir  wa Sheria  Chuo Kikuu  cha Zanzibar University   (SUZA) Dkt Sikujua Omar Hamad amesema kukosekana kwa  sheria hiyo imepelekea  kuwakosesha baadhi ya haki za wanafunzi waliopo chuoni hapo.

“Tumebaini kuwa sheria na kanuni za Chuo cha Mafunzo hazipatikani ipasavyo kwani   hata wao wenyewe hawazifahamu  sheria hizo ,hivyo fanyeni marekebisho ya sheria ili mupate  kuifahamu kwani bila ya kanuni hakuna sheria”,alisisitiza Mhahir Sikujua.

Amema  Sheria ya Chuo cha Mafunzo  haijulikani hata kwenye mitandao jambo ambalo linapelekea kufanya makosa kwa badhi ya Maafisa bila kujua   hivyo ipo haja ya kufanya kila jitihada ikiwemo kufika Baraza la Mapinduzi kuhakikisha sheria hiyo inapatikana na kutumika .

Aidha Mhadhir  amefahamisha kuwa mafunzo hayo yamelenga zaidi kujua miongozo ya Kitaifa ,Kimataifa na Kikanda  katika kuwasimamia wanawake wa Chuo cha Mafunzo kutakakopelekea Maafisa wa magereza  kujua vipi watawaongoza watuhumiwa  na wanafunzi ambao wapo Chuoni hapo.

Mhadhir ameeleza kuwa Mataifa ya nchi nyingi yamepiga hatua juu ya sheria  ukilinganisha na  sheria za huku jambo ambalo linarejesha nyuma jitihada za kimataifa katika kuwezesha wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo  kupata haki zao.

Nae  Afisa anaesimamia Miradi ya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia kutoka  (TAMWA) Zainab Salum Abdalla  amesema kuwa lengo la mafunzo hayo  ni kuwajengea uwezo wakufunzi kufahamu  namna gani wanaweza kuwasimamia wanawake waliomo katika Gereza kwa kuzingatia miongozo na sheria.

Nao washiriki wa mafunzo hayo  wamesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia  kupata uwelewa wa kujua mambo mengi ikiwemo haki ya  michezo na Ujasiriamali  kwa wanafunzi wao lakini wanashindwa na  nyenzo za kufanikisha kupatikana kwa haki hizo.

Hivyo wameiomba Serikali kuwasadia nyenzo zikiwemo za michezo ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapata haki yao ya ya kucheza  kwani kunabaadhi ya maswala hawewezi kuyafanikisha  bila ya kupata usaidizi.

Mafunzohayo ni ya siku mbili yameandaliwa na Chama cha Waaandishi wa Habari Wanawake TAMWA kwa kushirikiana  na Chuo cha Mafunzo.

 


Mhadhir kutoka Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Dk. Sikujua Omar akiwasilisha mada ya miongozo  ya  kitaifa,kimataifa na kikanda  katika kuwasimamia wanafunzi wanawake wa chuo cha mafunzo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Chuo hicho (Magereza)  juu ya  kuwaongoza wanafunzi  hao huko Makao Makuu ya Magerezo Kilimani Zanzibar,Julai 21,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...