* Washiriki kuchangia damu pia
UONGOZI wa shule ya sekondari ya Mary Goreti iliyoko Moshi, mkoani Kilimanjaro imeandaa zoezi la upimaji wa afya bure pamoja na uchangiaji wa damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Shule hiyo Sr Clementina Kachweka Jumanne, wakati akizungumzia swala hilo, ambapo alisema swala hilo linalenga kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.
“Maozezi haya mawili pia yataenda sambamba na usajili wa washiriki wa mbio za kilomita 5 na kilomita 10 ambazo zinaandaliwa kwa ajili ya kuboresha afya za watu, hii pia ikiwa ni sehemu za maadhimisho ya jubilee hiyo ya miaka 25 ambayo tunaendelea nayo”, alisema.
“Swala hili kwa njia moja au nyingine pia linalenga kurudisha kwa jamii ambayo tunafanya nayo kazi kwa miaka yote 25 tangu kuanzishwa kwa shule yetu”, alisema.
Mkuu huyo wa shule alisema zoezi la upimaji wa afya Bure na uchangiaji damu litakalofanyika July 7, 2023, katika viwanja vya shule hiyo ambapo wataalamu wa afya watapima magonjwa yasiyoambukiza kama vile ugonjwa wa kisukari, presha pamoja, uzito, macho na pia kupewa elimu kuhusu lishe bora na usafi wa mwili.
Sr Clementina aliendelea kusema matukio hayo ni sehemu ya menngine ambayo yatafuatilia ikiwa ni kuelekea kwa harambee kubwa ambayo inatarajiwa kufanyika Septemba 29, mwakani, mwaka ambao maadhimisho hayo yatafikia kilele chake.
Alisema, “Harambee hiyo itafanyika ili kuwezesha ukarabati wa maeneo mbalimbali ya shule yetu ambayo mwakani tunatarajia kuadhimisha jubilee ya miaka 25 tangu ilipoanizhswa mwaka 1999”.
Shule ya sekondari St Mary Goreti imekuwa na mwendelezo wa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na ugawaji miche ya miti 2000 ambayo tayari imeoteshwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ili kurudishia uoto wa asili na kuboresha mazingira.
Alisema upandaji wa miti ni mpango uliowekwa na uongozi wa shule hiyo kama maadhimisho hayo ili kuunga mkono juhudi za serikali zinaoendelea sasa za kuboresha mazingira hapa nchini ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo alisema katika kutekeleza azma hiyo, shule hiyo inashirikiana na benki ya NMB.
Alitoa rai kwa wananchi wote wakiwemo wazazi na wanafunzi, kuunga mkono juhudi za Serikali za kupanda miti kutokana na ukweli kuwa miti ni sehemu ya maisha ya Binadamu.
Shughli zote za St Mary Goreti za kuelekea sherehe za Jubilee zinaratibiwa na Kmapuni ya Executive Solutions Limted, ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza katika shughuli za habari na kuandaa matukio mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...