Mbunge wa Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 16/07/2023 ametembelea Kata ya Ngamiani Kati ambapo pia amechangia kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000/-) kwa vikundi vitatu vya Wajasiriamali ambavyo ni Nguvu Kazi kilichopo barabara 12 Mnadani, Mtaa wa Makoko; Kikundi cha Kuonda Mai cha Wafanyabiashara wa kuku kilichopo Sokoni Ngamiani na Kikundi cha Wazee kilichopo mtaa wa Maua. Kila kikundi, kimepatiwa kiasi cha shilingi milioni 2.
Aidha, Mh Mbunge amechangia shilingi laki 3 kwa ajili ya kukarabati Sehemu ya kufanya mazoezi ya ngumi kwa vijana katika mtaa wa Karafuu.
Mhe Ummy ameeleza kuwa licha ys majukumu ya kitaifa aliyonayo ataendelea kutimiza wajibu wake kikamilifu wa kuwatumikia wananchi wa Tanga Mjini hususani kutatua kero za maendeleo ya wananchi kupitia fedha za Serikali Kuu, Fedha za Halmashauri pamoja na mshahara wake na posho.
Akiongea baada ya kupokea mchango huo kwa niaba ya vikundi vingine, Ndugu Sadik Ali Mwenyekiti wa Kikundi cha Nguvukazi alimshukuru Mhe Mbunge kwa kuendelea kuwajali wananchi wake.
Katika ziara hii, Mhe Ummy aliongozana na Mhe Habibu Mpa, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kati, Mhe Fatuma Kitogo, Diwani wa Viti Maalum pamoja na Viongozi wa CCM ngazi ya Kata na matawi.
Imetolewa na;-
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini
16/07/2023
Home
HABARI
MBUNGE UMMY MWALIMU ACHANGIA MILIONI 6.3 KUWEZESHA WAJASIRIAMALI NA VIJANA NGAMIANI KATI JIJINI TANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...