Na Mwandishi Wetu

Wadhamini wakuu wa ligi ya Tanzania bara maarufu kama Ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya Biashara(NBC), imewapelekea wakazi wa jiji la Mwanza kombe jipya la ubingwa wa ligi hiyo namba tano kwa ubora barani Afrika.

Kwa mujibu wa NBC, lengo la kulipeleka kombe hilo mkoani Mwanza, ni kuwapa fursa wateja wa benki hiyo, wapenzi wa soka na wakazi wa jiji hilo kwa ujumla, fursa ya kulishuhudia na kupiga nalo picha kombe hilo jipya.

Shughuli ya kulishuhudia kombe, imeenda sambamba na fursa ya kupata huduma mbali mbali za kibenki kwa wakazi wa jiji hilo kutoka katika benki hiyo kongwe na yenye mtandao mpana wa matawi hapa nchini.

   wateja wake pamoja na mashabiki wa soka kombe hilo na kuwapa fursa ya kuliona na kupiga nalo picha.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC pamoja na mashabiki na wapenda soka wa mkoa wa Mwanza wakilifurahia  kombe la ligi kuu ya NBC ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa benki ya NBC ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi ya soka Tanzania bara kuwapelekea  wateja wake pamoja na mashabiki wa soka kombe hilo na kuwapa fursa ya kuliona na kupiga nalo picha.

Baadhi ya mashabiki na wapenda soka wa mkoa wa Mwanza wakilishuhudia kombe la ligi kuu ya NBC ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa benki ya NBC ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi ya soka Tanzania bara kuwapelekea  wateja wake pamoja na mashabiki wa soka kombe hilo na kuwapa fursa ya kuliona na kupiga nalo picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...