Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vivo Energy Tanzania, Grace Kijo (kushoto) akimkabidhi funguo ya Bodaboda mshindi wa promosheni ya Jaza Ushinde Tena na Engen kutoka Korogwe Tanga, Hatibu Kusaga aliyejishindia zawadi hiyo baada ya kushiriki kujaza mafuta kwenye vituo vya Engen na kuingia kwenye droo hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Korogwe.
Huu ni muendelezo wa promosheni hii itakayomalizikia mkoani Morogoro ambapo itatoa washindi wengine wiki hii, ili kushinda mteja anatakiwa kuweka mafuta kwenye vituo vya Engen na atakuwa ameingia kwenye droo hiyo.
Mshindi wa Runinga, Francis David akiwa na zawadi yake mara baada kukabidhiwa
Mshindi wa friji, Said Mambongo akiwa na zawadi yake mara baada kukabidhiwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...