Na.Khadija Seif,Michuziblog
SHINDANO la Bingwa Msimu wa pili latambulishwa Watu maarufu mitandao ya kijamii wajitosa , Washiriki 20 kuingia kambini Julai 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Leo Julai 18,2023 Jijini Dar es salaam, Meneja Mradi wa shindano hilo Ombeni Phiri amesema bingwa ni zaidi ya burudani ambapo msimu wa kwanza waliingia washiriki 18 ambao wengi wao ni vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na mmoja wao aliibuka mshindi na gari aina ya crown pamoja na pesa taslim.
Hata hivyo ameeleza lengo la kuwepo kwa shindano hilo ni kuwapa fursa vijana Kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo fursa zilizopo katika mitandao ya kijamii katika kukuza na kutengeneza brand zao.
Aidha kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kuwa kupitia Msimu wa kwanza walipokea maoni mbalimbali kutoka kwa watazamaji namna ambavyo wangependa msimu ujao uboreshwe kwa baadhi ya vitu na ndio sababu iliyopelekea mwaka 2022 kusiwepo kwa shindano hilo.
Pia amesema Shindano hilo ni daraja la kufunguka kwa fursa nyingi kwani Hata usipofanikiwa kushinda unaweza kupata fursa ya kuwa balozi wa Makampuni.
"Harmorapa alikua miongoni mwa washiriki kwa msimu uliopita hivyo kampuni ya Startimes iliweza kumpa ubalozi wa mwaka mmoja ambapo fursa ya ushiriki wake ilianzia hapo kuonekana hakutoka mtupu pamojana washiriki wengine walipata viinua mgongo vyao.
Pia Malisa amewaambia watazamaji wa bingwa kulipia visimbuzi vyao kwani msimu wa pili una maudhui tofauti tofauti yenye kufunza ambapo hata watazamaji watapata elimu mbalimbali.
Nae Mshindi wa Bingwa msimu wa kwanza Noel maarufu kama "Photogenic mtoto" amewaasa washiriki hao kuwa na nidhamu na kuendana na kauli mbiu ya shindano hilo isemayo "Najiamini kinoma" hivyo washiriki wanatakiwa kujiamini na kutumia fursa hiyo kutengeneza brand zao.
Hata hivyo Photogenic amewatia moyo washiriki hao wanapoianza safari yao ya mafanikio wawapo katika shindano hilo ambapo ingizo jipya la washiriki msimu huu wa pili kuna sura mbalimbali zenye ushawishi katika mitandao ya kijamii akiwemo Mchekeshaji Mkali wenu,Amirado pamoja na Mwanamitindo Hamid .

Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Wanahabari Leo Julai 18,2023 Jijini Dar es salaam mara baada ya kutangazwa kwa msimu wa pili wa shindano la Bingwa ambapo amewaambia washiriki kuwa shindano hilo linatoa fursa kwa Vijana wa kitanzania huku akiwataka watazamaji kulipia ving'amuzi vyao ili kushuhudia utofauti wa msimu huo wa pili uliosheheni watu mbalimbali wenye umaarufu kwenye mitandao ya kijamii
Meneja Mradi wa Shindalo la Bingwa Ombeni Phiri akizungumza na Wanahabari Leo Julai 18,2023 akifafanua zaidi kuwa msimu wa pili wa shindano hilo ni zaidi ya burudani ambapo washiriki 18 wataingia kambini julai 30,2023

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...