Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Bw. Frank Kanyusi amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam(DITF) kujisajili na kupata vyeti vya kuzaliwa papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari na wananchi waliojitokeza kupata huduma zinazotolewa na RITA kwenye maonesho hayo,Bw Kanyusi mbali ya kutoa wito huo amepongeza mwitikio wa watu wengi kujitokeza kwa wingi kujisajili na kupata vyeti vyao ambapo mpaka sasa watanzania zaidi ya elfu Tatu (3,000) wameshajisajili wa kipindi hiki cha maonesho.
“Elimu ambayo tumekuwa tukitoa kwa wananchi imekuwa na tija kwani wananchi wameelewa umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa na hivyo wamejitokeza kwa wingi wakiwa na viambatanisho vinavyoitajika na hivyo kufanya zoezi kuchukua mda mfupi,"alisema Bw. Kanyusi.
Alisema viambatanisho muhimu vinavyohitajika ili kufanikisha upatikanaji wa cheti hiko ni pamoja na kadi ya kliniki, pasi ya kusafiria, Cheti cha ubatizo, Cheti cha elimu ya msingi au Sekondari au vitambulisho vya kupiga kura au utaifa vya wazazi na kitambulisho cha kupiga kura au kitambulisho cha utaifa.
Alise cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu sana kwa kila mwananchi kwani ni utambulisho wa awali na kiambatanisho kinachomwezesha mwananchi kupata huduma mbalimbali ikiwemo elimu, matibabu, huduma za kifedha, ajira na kuwezesha kupata nyaraka nyingine za utambulisho kama kitambulisho cha taifa, Pasi ya kusafiria (passport) na nyinginezo.
Bw. Kanyusi lisema miongoni mwa huduma wanazozitoa ni pamoja na elimu kwa wananchi kuhusu huduma zote ambazo wakala anazitoa zikiwemo huduma ya usajili wa vizazi kwa wananchi ili wapate vyeti vya kuzaliwa sambamba na huduma ya msaada wa kisheria kuhusu masuala ya mirathi na kuandika Wosia.
“Usajili unaofanyika hapa Sabasaba unafuata miongozo na taratibu zote kama inavyofanyika katika Ofisi zetu na siyo kwamba kuna urahisi kama wengine wanavyofikiri. Fomu za maombi zikipokelewa na kuhakikiwa, zinapelekwa ofisini kwa ajili ya kuchakatwa na vyeti huandaliwa kwa yale maombi yaliyokidhi vigezo,"alisema Bw. Kanyusi .
Kwa upande wake, Bi Mary Ishengoma mnufaika wa zoezi hilo mbali ya kuipongeza kazi nzuri inayofanywa na RITA alisema juhudi ya kuhakikisha kila mtanzania anapata na cheti ni hatua nzuri.
“Kwa kweli zoezi la upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa hapa sabasaba limekuwa lakuvutia sana kwani watoa huduma wamekuwa wakitoa huduma kwa umahili na ufanisi na hivyo kufanya zoezi kuchukua muda mfupi,” alisema Bi. Ishengoma.
Naye Bw. Paul Munishi ambaye alishapata cheti cha kuzaliwa kwenye zoezi hilo aliwataka wananchi ambao bado hawana vyeti vya kuzaliwa kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo ili kunufaika na huduma zinazotolewa na RITA ikiwemo msaada wa kisheria bure kuhusu Mirathi na Kuandika wosia.
Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kwenda kujisajili ili kupata cheti cha kuzaliwa kwenye banda la wakala wa Usajili na Udhamini( RITA) kwenye maonesho yanayoendelea ya 47 ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu kwa Sabasaba jijini Dar es salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...