Wakala wa Usajili Ufilisi na Udahmini [RITA] imesajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa papo hapo kwenye Kilele cha maadhimisho ya sikukukuu ya saba saba iliyofanyika tarehe 07/07/2023 kwenye viwanja vya J.K Nyerere jijin Dar es Salaam.

Akiwakabidhi vyeti vyao vya kuzaliwa wananchi waliojitokeza kujisajili kwenye sikukuu hiiyo ya saba saba,Naibu Kabidhi Wasii Mkuu Bi Irene Lesulie amesema kuwa RITA imejipanga vizuri kuwapatia huduma Wananchi kiurahisi na kuwataka kutumia fursa hii kujitokeza kwa wingi kupatiwa huduma kwenye maonesho hayo.

"Nawasihi wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho haya ya saba saba ,maana tunasajili na kutoa vyeti hapa hapa uwanjan,yaani unajiandikisha leo na cheti unapata leo".

Aidha baadhi ya wananchi waliojitokeza kusajiliwa na kufanikiwa kupata cheti kwenye viwanja hivyo vya saba saba ambapo maonesho ya 47 ya maonesho ya biashara yanaendelea wameipongeza RITA kwa kuwarahisishia huduma kwa kuwapatia cheti siku hiyo hiyo!!!

"Hawa RITA wako vizuri kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa hapa hapa sio mchezo,kwa watu tulivyojaa sikutegemea kupata cheti leo,"Alisema Salma Ubuguyu mmoja wa wananchi waliojitokeza kupatiwa cheti cha kuzaliwa

RITA inaendela kutoa Huduma ya Usajili wa vyeti vya kuzaliwa,Elimu ya Mirathi Kuandika na kuhifadhi Wosia kwenye maonesho hayo hadi tarehe 13 Julai 2023 .
Wanachi wakichua vyeti katika banda la (RITA)

Wakazi wa Jijini la Dar es Salaam wakiwa kwenye banda la (RITA)

Mwananchi akipokea Cheti cha kuzaliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...