Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Angella Kairuki amesema Serikali wanapongeza michuano ya Ndondo CUP kwa namna ambavyo inaendelea kuibua vipaji kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Kairuki ametoa kauli hiyo leo kwenye Uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua rasmi michuano ya Ndondo CUP kwa mwaka huu wa 2023 ambapo pia wadau na mashabiki wa soka wameshuhudia uzinduzi huo.
Akieleza zaidi uwanjani hapo Waziri Kairuki amesema mashindano ya Ndondo CUP katika kipindi cha miaka 10 wamefanya kazi kubwa na nzuri ya kuendeleza sekta ya michezo kwa kuibua wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.
"Serikali tunaipongeza Ndondo Cup kwa namna ambavyo wamendelea kuibua vipaji lakini vile vile na namna ambavyo wameendelea kuviendeleza kwa miaka zaidi ya 10 wameweza kuibua vipaji zaidi ya wachezaji 20, 000...
" Lakini hapo hapo zaidi ya wachezaji wenye vipaji 50 wamesajiliwa na vilabu vikubwa mbalimbali ndani na nchi na nje ya nchi na naamini watakuwa wadau wa muhimu sana wa Ndondo Cup yenyewe lakini watakuwa wadau na wabia wa M-Mama pamoja na Michezo kwa ujumla wake.
Pia Waziri Kairuki ameishukuru benki ya CRDB lakini pia uongozi wa Clouds kwa uwekezaji ambao wameufanya pamoja na M mama kupitia Vodacom, Serikali na uongozi mzima wa Dar es Salaam pamoja na Wilaya ya ubungo kwa kushiriki kufanikisha michuano hiyo.
"Tukio hili la leo ni kubwa , wapo ambao wanaoshangaa Ndondo Cup inachezwa kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama na mtoto ,M Mama ni kitu gani ? Kwa hiyo kwa kipekee niwashukuru Ndondo Cup kupitia Shafii Dauda pamoja na uongozi mzima wa Ndondo Cup
"Pia niwashukuru CRDB Foundation pamoja na Embeju kwa kuasisi wazo hili kuweza kuona umuhimu wake lakini vile vile kwa watalaam wetu wa M - Mama , program Coordinator ambaye anaratibu programu nzima kwa niaba ya Serikali na Vodacom kwa kazi nzuri na kubwa wanayofanya
"Ukiangalia tangu tulipoanza programu ya M - Mama kama ambavyo Mkuu wa Mkoa ameendelea kusema ni programu mhususi ambayo iliasisiwa na tunamshukuru muanzilishi wake ni Rais DK .Samia Suluhu Hassan ambaye aalitoa baraka kubwa mwaka 2022."
Amefafanua ndani ya kipindi kifupi akina mama na watoto wachanga 21000 wameweza kupata huduma hiyo lakini maisha ambayo yameweza kuokolewa kwa zaidi ya maisha 741 na hapo walikuwa wapo katika mikoa michache tu.
Waziri Kairuki amesema mahitaji bado ni makubwa katika kuhakikisha maisha ya mama mjamzito na mtoto mchanga yanaokolewa , khiyo kwa kipekee anaishukuru Ndondo Cup kwa kuona umuhimu huo kwasababu mahitaji bado yataendelea kuwa ni makubwa sana kwa sasa wamefikia mikoa 18 lakini mpaka Oktoba mikoa yote 26 Tanzania Bara itakuwa imefikiwa pamoja na mikoa yote ya Zanzibar pia
"Kwa hiyo tunawashukuru pia CRDB Foundation pamoja na Ndondo Cup kwa kuwekeza fedha zao na hasa asilimia 10 ya mapato yatakayopatikana katika mechi za Ndondo Cup lakini pia kila udhamini watakaupata basi asilimia 10 zitatengwa.
"Ni Imani yangu kupitia michezo na wadau wengine pia wataendelea kujitokeza na kuweza kutenga mapato wanayoyapata katika kusaidia mambo muhimu, " amesema Waziri Kairuki
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albart Chalamila ameeleza kuwa Michuano ya Ndondo Cup muhimu katika mkoa huo huku akitoa rai kwa klabu zote nchini na wao wawe mabalozi wazuri kupitia Ndondo Cup.
"Kwasababu kupitia hapa ndipo wanapoweza kuona vipaji vizuri na wanaweza kuwaeneeleza zaidi mpaka kwenye klabu zao, " amesema Chalamila huku akitumia nafasi hiyo kueleza umefika wakati uwanja wa Kinesi ufanyiwe matengenezo kwani umechakaa.
"Nikuombe Waziri Kairuki umeona uwanja wetu wa Urafiki ambao upo chini ya umiliki wa Serikali lakini kupitia Urafiki ukweli uwanja huu ni chakavu na mpaka muda huu unahitaji kuboreshwa kwa kiasi kikubwa. Ni vema tukakaaa sisi na Urafiki lakini kwa miongozo yako ili tuweze kuukarabati uwanja huu kupitia wadau.
" Na mwisho wa siku kama ulivyoona kuna uhitaji mkubwa wa viwanja vya michezo hapa kwetu Dar es Salaam na muda sio mrefu tunajiandaa pengine kuwa wenyeji wa mashindano mengine makubwa yanayohitaji kuwa na viwanja, "amesema.
Hivyo ametoa ombi kwa Waziri na atapeleka kwa barua ili watu wa Dar es Salaam wakae pamoja na wenzao wa Urafiki ili sasa waone namna gani viwanja hivyo chini ya Halmashauri au Manispaa ya Ubungo wavikarabati kupitia wadau kama CRDB.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Angella Kairuki(katikati) akipiga mpira kuashiria kuanza rasmi kwa michuano ya Ndondo Cup katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Angella Kairuki akisalimiana na wachezaji baada ya kuzindua michuano ya Ndondo Cup katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam
Sehemu ya mashabiki wa michuano ya Ndondo Cup wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI Angella Kairuki( kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya CRDB Majid Nsekela wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa uwanjani hapo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...