Na John Mapepele
Serikali
imetambua na kumpongeza Balozi Nguli wa utalii wa Tanzania nchini
Marekani mwenye umri wa miaka 63 bwana Macon Dunnagan kwa kuandika
historia ya kukamilisha kupanda mlima Kilimanjaro mara 50 hivi na
kuendelea kuitangaza Tanzania kimataifa hususan Marekani.
Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari akiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini leo mjini Moshi siku moja baada ya
kumaliza kushuka katika mlima huo kwenye safari yake ya mara ya 50
Dunnagan ametoa wito kwa watanzania na wageni kutoka sehemu mbalimbali
kuwa na tabia ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini Tanzania ili
kujionea utajiri wa vivutio mbalimbali ambavyo havipatika sehemu
nyingi duniani.
Aidha amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na
vivutio vingi ikiwa ni pamoja na wanyama wa aina zote wakiwemo Simba
Tembo Twiga na Chui pia kupanda Mlima Kilimanjaro.
Balozi
Dunnagan ambaye alianza kupanda mlima Kilimanjaro toka mwaka 1999
amesema ataendelea kuiamasisha Dunia kuja kuona maajabu ya vivutio vya
Taifa la Tanzania.
Akiongea kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini
amesema Serikali itaendelea kutambua michango ya watu wote wanaotangaza
utalii wa Nchi wa ndani na wanje akiwemo Macon.
Amempongeza
balozi huyo kwa kutoa hamasa kubwa wa watanzania na wamarekani kupitia
vyombo mbalimbali vya habari vya nchi hiyo ambapo amefafanua kuwa
Dunnagan alianza kuhamasika kupanda mlima Kilimanjaro mwaka 1967 baada
ya kuangalia movi ya “Snow of Kilimanjaro”.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...