-Umegharimu zaidi ya bilioni 13/-, uzalishaji kuanza mwaka 2025

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Uendelezaji Joto Ardhi Tanzania(TGDC) imesema tayari mtambo wake wa kuchoronga visima vya kuzalisha nishati ya jotoardhi ambao umenunuliwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 13 upo nchini.

Kwa mujibu wa TGDC mtambo huo kwa sasa umeshafika mkoani Mbeya na kinachosubiriwa ni mzabuni wao kufanya kamisheni ili mtambo huanze kufanya kazi huku ikielezwa matarajio yao ifikapo mwaka 2025 wawe wameanza kuzalisha umeme unatokana na nishati ya jotoardhi itakayoingizwa kwenye gridi ya taifa.

Akizungumza katika la TGDC lililopo kwenye banda la TANESCO katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa(Sabasaba) jijini Dar es Salaam Ofisa Mkuu wa Mawasiliano TGDC Khadija Faru amesema kupatikana kwa mtambo huo kunakwenda kuongeza kasi na ufanisi katika shughuli zao za kuchimba mashimo(visima) ili kupata nishati ya jotoardhi.

“Tuko kwenye maonesho haya yenye kauli mbiu isemayo Tanzania mahali sahihi kwa biashara na uwekezaji.Kauli mbiu hii imeendana na TGDC ambayo ni kampuni tanzu ya TANESCO .Tunaishukuru Serikali Awamu ya sita kwani TGDC ilikuwa na kiu ya muda mrefu kupata mtambo wake wa kuchoronga visima ili kupata nishati ya joto ardhi.

“Kupatikana kwa mtambo huu unakwenda kutuongezea kasi na hivi tunavyozungumza mtambo huu tayari umeshafika mkoani Mbeya,”amesema na kuongeza mtambo huo unakwenda kusaidia pia kukamilisha miradi mitano ya kimkakati.

Ameitaja miradi hiyo ni mradi wa nishati ya joto ardhi Ngozi ambao ndio wanakwenda kuanza kuchoronga kwa kutumia kutumia mtambo huo kwa mara ya kwanza kabisa.

Amesema baada ya hapo utafuata mradi wao uliopo Songwe ambao ukikamilika wanatarajia kupata megawati 5 mpaka mgewati 38 na baadae watakwenda kuchimba kwenye mradi wa Kijombaka unaotegemewa kuzalisha megawati 60 za umeme.

“Tukitoka hapo tutaenda Ruhoi Pwani katika mkoa Pwani ambako kuna sehemu moja tu na kisha tutamaliza kuchongora mradi wa Natron uliopo mkoani Arusha.Kote huko huu mtambo utaturahisishia kwasababu kuukodi gharama yake ni kubwa.

Amefafanua lengo ni kutekeleza azma ya Serikali kupata vyanzo mchanganyiko vya umeme ambapo kwa joto ardhi ni nishati salama ,safi , nafuu na rafiki wa mazingira huku akisisitiza ni nishati ambayo haina kiangazi wala masika kwani inapatikana wakati wote.

“Amesisitiza kuwa malengo ni kupata megawati 200 ambazo ndizo zitaanza kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.Umeme wa jotoardhi baada ya kuuzalisha matumizi yake ni yale yale,sisi ni watoto wa TANESCO hivyo umeme huu utaingizwa kule kule na kusambazwa kwa wananchi, maofisini na viwandani,"amesema Faru.

Ametumia nafasi hiyo kueleza TGDC inawakaribisha wawekezaji kwenda kuwekeza katika eneo la nishati ya Jotoardhi ambayo ni nishati nafuu salama na ni rafiki wa mazingira hasa kipindi hiki ambacho duniani kote inasisitizwa kutumia nishati safi kama njia mojawapo ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Ofisa Mkuu wa Mawasiliano katika Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania( TGDC) Khadija Faru akielezea mtambo wa kuchoronga visima vya nishati ya jotoardhi ambao umenunuliwa na Serikali kwa fedha zaidi ya Sh.Bilioni 13

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...