Na Mwandishi Wetu, Michuzi Blog

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema kitendo kilichofanywa na mtaalam wa afya katika Hospitali ya Kivule jijini Dar es Salaam anayeonekana katika video inayosambaa mtandaoni akiwa anasafisha vifaa vya hospitalini kwa njia isiyo rasmi ni kinyume na utaratibu na hakikubaliki.

Akizungumza kuhusu video ya tukio hilo , Waziri Ummy Mwalimu amesema tayari viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wameanza kulifanyia kazi suala hilo na watatoa taarifa rasmi.

Amefafanua kwamba kitendo hicho cha kusafisha vifaa vya hospitali kwa njia isiyosahihi ni kinyume na taratibu na miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi.

Waziri Ummy ametoa shukrani na pongezi kwa mwananchi alierekodi na kuisambaza clip hiyo na kutoa mwito kwa wananchi kuendelea kuibua mambo kama hayo yanayotokea katika vituo vya kutoa huduma za afya vya umma na binafsi ili kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa Huduma za Afya nchini.

Ametoa rai kwa wataalamu wa afya kuzingatia mafunzo na miiko ya kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea huku akisisitiza Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI wataendelea kuchukua hatua ili kuimarisha ubora wa huduma.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...