JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia vijana watatu wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kumbaka mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kishimba (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 14 aliyekuwa akitoka dukani kwenda nyumbani.

Akizungumza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi amesema limetokea Julai 8, mwaka huu saa  mchana katika Kijiji cha Igumhwa  kilichopo Kata ya Kitwana Manispaa ya Kahama.

Magomi amewataja watuhumiwa hao ni Dotto Venancy (18), Juma Mwita (17) na Paul Peter (17) ambao wanadaiwa kuhusika kumshambulia binti huyo.

Hata hivyo imebainika kuwa chanzo cha tukio hilo ni mmomonyoko wa maadili huku ikielezwa mmoja wa watuhumiwa hao ametoroka baada ya kutenda kosa hilo.Ameiomba jamii kujenga ukaribu na watoto wao kwa kuwalea katika maadili ya kidini na hofu ya Mungu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...