Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Julai
12, 2023 Jijini Dar es Salaam, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi
wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui.
Mazungumzo yao
yalikua na lengo la kushirikiana baina ya Nchi hizo mbili katika Sekta
ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambapo Ufaransa kupitia Balozi huyo,
ipo tayari kuleta Wataalam wa michezo mwezi Septemba mwaka 2023 kwa
ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa hapa nchini.
Mhe. Chana amewakaribisha katika Chuo Cha Michezo Malya na Butimba ambapo kuna wanafunzi wanaosoma michezo.
Mhe. Chana ameongeza kuwa Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Ufaransa imeanzisha Kituo cha kujifunza lugha ya Kiswahili.
Kwa
upande wa Balozi Nabil Hajlaoui amesema nchi yake inaendelea kukuza
Lugha ya Kiswahili ambapo amesema nchi hiyo ipo tayari kuunga mkono
ujenzi wa Shule Kiswahili hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...