Na Eleuteri Mangi, WUSM, Zanzibar


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza wizara zenye dhamana ya lugha ya Kiswahili kusimamia kikamilifu mkakakti wa kukuza na kubidhaisha lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Julai 6, 2023 wakati akizindua maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo yatafanyika kitaifa Julai 7, 2023 Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Amezitaja Wizara hizo kuwa ni; Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

“Andaeni nafasi za Watanzania kufundisha Kiswahili katika nchi mbalimbali duniani, kila mmoja awajibike kuhakikisha Kiswahilli kinakua na kuendelezwa, nimefurahi sana wanafunzi walivyotumia lugha ya Kiswahili kuandika insha ambazo leo hii nimewatunuku zawadi ya ushindi kwa kazi zao”, amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema yeye na Waziri mwenzake mwenye dhamana ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Tabiia Maulid Mwita wameahidi kutekeleza kwa ufasaha dhamana waliyopewa.


Dkt. Chana ameongeza kuwa, chimbuko la Kiswahili ni Tanzania na kwa sasa Watanzania idadi yao ni zaidi ya milioni 61 ambapo vijana ni zaidi ya asilimia 50 ambao wanapaswa kujengewa uelewa wa matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili ambacho kina fursa nyingi za ajira za ukalimani, watafsiri, waandishi wa vitabu pamoja na kazi za ubunifu.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...