
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na waandishi habari katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisaini vitabu vya mabanda yaliyoshiriki maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*Asema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka ya neema kwa kila sekta
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Serikali imesema kuwa sekta ya Ufugaji na Uvuvi ni utajiri mkubwa hivyo Watanzania watumie fursa hiyo katika kutengeneza kipato chao pamoja na kuongeza pato la Taifa.
Hayo aliyasema Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Ulega amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka msukumo mkubwa wa kuona mabadiliko katika sekta ya Mifugo na Uvuvi.
Amesema msukumo huo wa Rais ni kuona vijana na wanawake wengi wanaingia kwenye sekta hizo mbili katika malengo ya kutengeneza kipato pamoja kuongeza pato la Taifa kwa rasilimali zilizopo.
Ulega amesema katika kwenda kasi kwenye sekta wamekubaliana kuingia kwenye mpango wa BBT 'Building Better Tommorow' kwa ajili kuwaandaa vijana kufanya biashara ya ufugaji na uvuvi kibiashara sio kufuga kwa mazoea.
Amesema mpango BBT kwa vijana wanaotaka kunenepesha Ng'ombe na kuuza watafanya hivyo na soko lake liwa wazi ndani na nje ya nchi.
aenye malengo ya kunenepesha ngombe na kuuza na wale wataofuga samaki.
Hata hivyo amesema kuwa yote hayo ya kufanya bisahara ya ufugaji na Uvuvi wa kisasa kilichofanyika ni kuwaondoa katika zana duni na kwenda na zana za kisasa.
Amesema kwa ukanda Pwani uko katika ufugaji wa Kaa na Majongoo Bahari kutokana kuwepo kwa soko la uhakika kwa bidhaa hizo.
Amesema Wizara imejipanga kuhakikisha pato taifa linakua kutokana na rasilimali zilizopo katika Bahari na Maziwa zinatumika ipasavyo
Aidha katika mwaka wa Fedha 2022/2023 Serikali ilinunua ulipata boti 160 ambazo wanakwenda kuwapa Wavuvi bila kuwa na riba yeyote.
Amesema boti hizo zina uwezo kuweka kuhifadhi samaki Tani moja na zina GPS ya kuonyesha wapi anakwenda na wapi anatoka.
Waziri Ulega amesema rasilimali za bahari na maziwa hazijaweza kufikiwa kutumia boti hizo zitasaidia wavuvi kufika na kuwa na uhakika wa uvuaji samaki hao.
Amesema serikali ina mpango kutengeneza maumbo katika bahari kuvutia samaki ili mvuvi asiende mbali kuwinda samaki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...