ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Maimbo Mndolwa ametoa ya moyoni mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan sambamba na kuelezea namna Rais anavyopigwa nyundo na kutupiwa maneno mengi.
Akizungumza leo Agosti 15,2023 wakati wa uzinduzi wa jengo la kitega uchumi la Kanisa la Anglikana Tanzania ,Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma , Askofu Mkuu Dk.Mndolwa pamoja na mambo mengine ameeleza namna ambavyo Kanisa hilo linashirikiana na Serikali yangu kuanzishwa kwake katika kutekeleza miradi mbalimbali na kusaidia jamii yenye uhitaji.
Wakati anaanza kuzungumza Askofu Dk.Mndolwa amesema yeye amefika hapo na kuupata Udaktari wa Falsafa kupitia mikono ya wajomba zake ambao wote ni Waislamu.
“Nimesoma kupitia michango yao.Mheshimiwa Rais Kanisa la Anglikana tangu kuanza kwake mpaka muda huu miaka yote limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali …
“Na sisi wakati wote tunapofanya ibada tumekuwa tukiiombea Serikali lakini na kukuombea wewe mwenyewe(Rais) leo umetupa heshima ya kipekee kama kawaida yako, nyakati zote tulipoomba kuwe nawe hukusita kuungana nasi.
“Lakini leo kipekee sana ulijua unashughuli nyingi lakini hata kwa kushtukizwa tumefurahi kukuona kwa mara nyingine Mungu aendelee kukubariki sana. Rais Kanisa halifanyi kazi za Injili tu kama ulivyoshuhudia mwenyewe hapa.
“Tunafanya kazi za maendeleo lakini na kazi za kijamii,umeshuhudia vijana wetu hapa wenye tatizo la kuona lakini ukifika kule Iringa tuna watoto na vijana wetu ambao wana shida ya viungo, ukifika pale Mkono Handeni tuna vijana wenye shida ya viungo,”amesema.
Ameongeza Muheza wanacho kituo kinalea watoto 320 wanaioshi na magonjwa na hayo yote wanayafanya wakijua hakika ya kwamba mkono wa Mungu unagusa watu kwa njia njia nyingi na njia moja ya kufanya hayo ni kugusa maisha ya wenye uhitaji mkubwa.
“Ili uweze kuyafanya hayo yaweze kwenda vizuri unahitaji fedha na fedha haziji kirahisi kama hukutafuta mkondo wa maji wa kuzileta.Hapa tunaposimama tuipongeze sana Dayosisi ya Centre Tanganyika kwa kuweka mkondo huo wa kuleta fedha hizo.
“Najua Baba Askofu Chilongani haikuwa rahisi kuanza , na mara nyingi tumekuwa tukishauriana .Baba Askofu pole kwa yote uliyopitia ni magumu kweli kweli, nyundo kweli kweli…
“Lakini hatimaye wote leo tunafurahi kama ambavyo naamini hata leo Mheshimiwa Rais Samia anapigwa nyundo nyingi na maneno mengi lakini mwisho wa siku ni sisi tutakaopita kwenye barabara hizo, ni sisi tutakaopita kwenye lami.
“Ni sisi tutakaopanda kwenye ndege , ni sisi tunaopanda kwenye meli.Kwa hiyo tunawaombea na mjue kanisa linawaombea na niwatie moyo Kazi mnayofanya pamoja na maumivu na maneno mengi Mungu anaona msikate tamaa,”amesema Askofu Dk.Mndolwa.
Amesisitiza ni hivyo hivyo kwa Makasisi na Mashemasi wameona nyota imeanza hivyo wasirudi nyuma huku akifafanua pasiko na kusemwa ujue hakuna kufanya kazi.
Ameongeza palipo na kazi yenye nguvu lazima maneno yatainuka na siku zote ushindi unapatikana pale wanaposimama na Mungu.“Mheshimiwa Rais kwa mara nyingine tunakushukuru na Mungu aendelee kukubariki sana.”
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Maimbo Mndolwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...