Na John Walter-Manyara

Halmashauri ya wilaya ya Babati ipo mbioni kutumia Teknolojia mpya ya Fensi ya Umeme kuzuia Wanyama waharibifu kuvamia makazi na mashamba ya watu wanaoishi pembezoni mwa hifadhi.

Hatua hiyo inakuja baada ya Taasisi ya Chemchem kuwapeleka viongozi mbalimbali wa Vijiji 10 kujifunza katika wilaya ya Serengeti namna walivyowadhibiti Wanyama kupitia uzio. Teknolojia hiyo imeletwa  nchini na Ikorongo Grumeti Game Reserve iliyopo kijiji Cha Rwamchanga wilaya ya Serengeti mkoani Mara.  

Kwa Niaba ya Serikali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya ameubariki mpango huo na kuahidi kulipeleka suala hilo kwenye baraza la Madiwani ili utekelezaji uanze mapema.

Amesema Teknolojia hiyo itawawezesha wakulima wa kata za Nkaiti, Mwada na Magara zenye vijiji 10 zilizopo pembezoni mwa hifadhi kupata mavuno ya kutosha hivyo kuongeza kipato kwa familia na serikali kwa ujumla.

Diwani wa kata ya Nkaiti inayokabiliwa na changamoto ya uvamizi wa Wanyamapori Steven Mollel, amesema mpango ukifanikiwa katika Vijiji vyao itasaidia kupunguza malalamiko kwa Serikali na gharama za fidia.

Mwenyekiti wa wa wenyeviti wanaounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge (WMA) Wilaya ya Babati Daudi Melengori amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wakiichukua teknolojia hiyo kwa uzito, kilio Cha wakulima kitafika mwisho.

Mwekezaji kutoka Taasisi ya Chemchem Nicholaus Nigre amesema yupo tayari kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya utalii na Kuwalinda wananchi dhidi ya wanyama wakali  kwa kuweka fensi hiyo kuzunguka Jumuiya.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...