KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia Bw. Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Pamoja na Mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yamejikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Indonesia katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo, afya, elimu na nishati.

Balozi Shelukindo amemhakikishia Katibu Mkuu huyo ushirikiano wa dhati katika kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu na na Indonesia. Aidha, amemueleza kwamba mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni mazuri na salama na kuwasihi wawekezaji kutoka Indonesia kuchangamkia fursa zilizopo.

Naye, Bw. Herawan amepongeza uhusiano imara uliopo baina ya serikali hizi mbili (Tanzania na Indonesia) na kuongeza kuwa Indonesia itaendelea kushirikina na Tanzania katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya nchi zote mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumza baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...