Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Mohammed Bin Zayed Al Nahyan katika Ikulu ya nchi hiyo (Qasr Al Watan) iliyopo mjini Abu Dhabi.
BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed mapema wiki hii amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Mohammed Bin Zayed Al Nahyan katika Ikulu ya nchi hiyo (Qasr Al Watan) iliyopo mjini Abu Dhabi.
Viongozi hao pia walipata wasaa wa mazungumzo ambapo Mheshimiwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu alimhakikishia Mhe. Mohamed ushirikiano wa Serikali yake katika kutekeleza majukumu yake nchini UAE kwa manufaa ya pande zote mbili hususan kiuchumi.
Kwa upande wa Balozi Mohamed alimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa atahakikisha Watanzania na Waemirati wananufaika na fursa za uchumi zilizopo pande zote mbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...