KAMPUNI ya bima ya Strategis imetoa wito kwa wakulima kote nchini kuyat TVumia maonyesho ya kilimo ya Nanenane (Siku ya wakulima) ambayo yalifikia kilele chake Agosti 8, kuendelea kupata elimu ya aina mpya ya bima ya kilimo ya Mtetezi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Strategis- bima za majanga na mali, Bw. Jabir Kigoda amesema huu ni wakati muafaka kwa wakulima kupata elimu zaidi kuhusiana na bima hii jambo ambalo amesema litawaongezea maarifa kwenye shughuli zao za kilimo.

"Elimu hii ni kwa faida yao kwani wanachohitaji ni kuwa katika vikundi kwani hatutoi huduma hii kwa mtu mmoja mmoja, bali kwa njia ya vikundi ambayo ni gharama nafuu kwa wakulima," alisema.

Alisema watatoa elimu hiyo katika maeneo mbalimbali nchini ambako wakulima wanajumuika.

"Mikoa mbalimbali iliadhimisha siku hii ya wakulima kwa namna ya pekee kupitia kanda zao husika, elimu kuhusu bima hii mpya ambayo wakulima wengi wamekuwa wakiisubiri baada ya kupata hasara kwa miaka mingi zinazotokana na majanga mbalimbali itaendelea kutolewa- kwa ufasaha nchi nzima”, alisema.

Aliendelea kusema kuwa ujio wa bima ya Mtetezi kunatimiza ndoto ya wakulima wengi na kwamba imekuja wakati muafaka ambapo wanaadhimisha mafanikio yao na kuangalia jnsi ya kuboresha mafanikio hayo.

Alisema mchango wa Mtetezi katika malipo ya jumla kwa mwaka wa 2021 ulikuwa n takribani asilimia 1 ambayo na kwamba ni muda muafaka sasa kwa wadau wote wakuu kukusanyika ili kukuza bima hii.

“Upo Uwezekano mkubwa wa kupata mafanikio haya; ninaamini kampuni ya bima ya Strategis, ina jukumu la kuhakikisha wakulima wanapata kile wanachokihitaji”, alisema.

Alisisitiza kwa kusema kuwa faida za bima ya Mtetezi ni pamoja na ulinzi wa fedha, usimamizi wa vihatarishi aina mbalimbali kwenye selkta ya kilimo, uboreshaji wa upatikanaji wa mikopo, uendelevu wa biashara, kuhimiza uwekezaji katika kilimo na kuhakikisha utulivu wa mawazo kwa wakuulima.

Aidha alibainisha kuwa bidhaa hiyo mpya imeanzishwa ili wakulima wapate huduma bora za bima a kilimo ili waweze kukabiliana na athari aina zote kama vile ukame, mvua ya mawe, mafuriko, baridi kali, upepo mkali, wadudu wanaoathiri mazao na magonjwa pamoja na nyongeza ya hiari ya Bima ya Hali ya Hewa ambayo kimsingi hushughulikia changamoto ya mafuriko na ukame.

Bima ya kilimo ya Mtetezi kwa kawaida hugharamia mazao mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mazao makuu kama vile Nafaka, Mbegu za Mafuta, Mikunde, mazao yenye asili ya mizizi, zao la miwa kwa ajili ya uzalishaji wa Sukari na mazao aina mbalimbali ya kibiashara.

Kampuni ya Bima ya Strategis imekuwa katika soko la bima kwa zaidi ya miaka 20. Kwa sasa kampuni hiyo ina matawi tano (5) hapa nchini ambayo ni pamoja na Mwanza, Zanzibar, Arusha, Dodoma na Dar es Salaam. Mbali na Bima ya kilimo ya Mtetezi, kampuni ya bima ya Strategis pia inatoa bidhaa zingine za bima kama vile Bima ya Magari, Bima za usafirishaji bidhaa wa aina mbalimbali majini, angani na ardhini, Bima ya mali, Bima ya vyombo vya Baharini, Bima ya Matibabu na bima aina nyingine mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...