Na Pamela Mollel,Arusha 

Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakabete amewataka vijana wanaochuana katika mashindano ya soka ya Chuga Cup kufanya bidii ili kuibua vipaji vyao.

Akizungumza katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo iliyozikutanisha timu za Engutoto na Kaloleni zilizomalizika kwa kutoshana Nguvu ya 0-0, Mwakabete alisema michuano hiyo itasaidia vijana katika kuwaibua kisoka ili waweze kuonekana na hivyo itachangiwa na juhudi na bidii katika michezo hiyo.

"Na mimi kule jimboni kwangu Busokelo nanzisha mashindano kama haya ndani ya mwezi wa tisa mwaka huu hivyo tutakaa na kamati mshindi atakaetoka huku kwenye ligi hii aje apambane na bingwa katika   mashindano na timu itakayoshinda na naamini makombe nitachukua mimi,"alisema Mwakibete.

Alimpongeza mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo kwa kuona na kuanzisha michuano hiyo katika kuwaibua vijana.

Naye Mrisho Gambo ambaye ni Mbunge wa Arusha mjini alisema "Tuliamua kuanzisha mashindano ili kuweza kutoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao kwani wapo weengi wenye uwezo na  wamekosa fursa ya kuonyesha vipaji vyao  na hapa tumeshirikisha timu 32  kutoka  Arusha mjini, Monduli,Longido na Arumeru.

Mashindano ya Chuga Cup yamedhaminiwa kwa  gharama ya shilingi milioni 180/- ambayo ina maana ya milioni 60/- zinazotolewa kwa ARFA kila mwaka kuendesha ligi hiyo kwa miaka mita.

Bingwa wa Chuga Cupa atajinyakulia millioni 5, mshindi wa pili Milioni mbili, mshindi wa tatu Milioni moja .

Zawadi nyingine zitatolewa kwa wanamichezo bora ikiwa ni pamoja na mfungaji, mchezaji bora na mwamuzi bora.

.Katibu wa chama cha soka mkoa Arusha (ARFA) Emmanuel Anthony alisema hatua ya makundi itamalizika Septemba 7 na baada ya hapo hatua ya 16 bora itafuata.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...