Katika kuhakikisha Vijana wanamaliza safari yao ya masomo bila vikwazo, hususan vinavyohusiana na afya na ustawi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni - UNESCO kupitia mradi wake wa Haki Zetu, Maisha yetu, Mustakabali Wetu (“Our Rights Our Lives Our Future Plus”) unaofahamika kama O3 Plus likishirikiana na Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa (ILO) limekutanisha wawakilishi wa wizara ya elimu na wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Vyuo vikuu 14, wataalam wa sera ya usalama na afya kazini kutoka TUKTA na Tume ya Taifa ya UNESCO (NATCOM) katika kikao kazi cha siku 5 kinacholenga kuimarisha/kuboresha na kuandaa sera za afya na ustawi kwaajili ya vyuo vikuu Tanzania.
Uboreshwaji wa sera zinazolenga kuimarisha afya na ustawi wa wanafunzi na wafanyakazi vyuoni umetokana na mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti ya UNESCO (O3 Plus Baseline report, 2022) ambayo ilionesha baadhi ya vyuo havina sera hizi, na vile vyenye sera, sera zake hazijitoshelezi kulingana na mazingira ya sasa.
Mchakato huu utanufaisha vyuo vikuu 14 ambavyo ni:
University of Dar es Salaam (Mlimani campus), Dar es Salaam University College of Education (DUCE), Mkwawa University College of Education (MUCE), University of Dar es Salaam-Mbeya College of Health and Allied Sciences (MCHAS), Institute of Marine Sciences (IMS) in Zanzibar, Mineral Resource Institute (MRI), University of Dodoma (UDOM) , Mwalimu Nyerere Memorial Academy University, Institute of Rural Development Planning (IRDP) Mwanza, St. Augustine University of Tanzania (SAUT) Mwanza, University of Iringa (UoI), Ruaha Catholic University (RUCU), Tanzania Institute of Accountancy (TIA), and Kampala International University in Tanzania (KIUT)
Sera zinazoenda kuboreshwa na kuandaliwa ni pamoja na:
i. Sera ya Ustawi wa wanafunzi (Students’ welfare policy)
ii. Sera ya kupinga unyanyasaji wa kingono (Anti-sexual harassment policy)
iii. Sera ya masuala ya Jinsia (Gender policy)
iv. Sera ya Afya (Health policy)
Mradi wa O3 Plus, umekua ukitekelezwa kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja hadi sasa, katika vyuo vikuu 17 Tanzania bara (15) na Zanzibar (2).Katika kipindi hiki zaidi ya wanafunzi 100,000 wa vyuo vikuu wamekua wakinufaika na afua mbalimbali za mradi ikiwemo uanzishwaji na usimamizi wa madawati ya jinsia vyuoni (14), utoaji wa Elimu rika (Providers-led Peer Assisted Program), utoaji wa kozi mtandao ihusuyo elimu ya kina ya stadi za maisha zinazozingatia VVU/UKIMWI, Afya ya uzazi na jinsia (CSE), Uboreshwaji wa vituo vya kutolea huduma za Afya kwa vijana vyuoni, pamoja na utoaji wa mafunzo kwa watoa huduma za afya juu ya utoaji wa huduma rafiki za afya kwa vijana.
Mratibu na msimamizi wa mradi Tanzania Bw. Mathias Luhanya anasema:
“ Lengo la mradi ni kuboresha mazingira ya vyuo ili kuhakikisha Vijana wana Afya na Ustawi bora na wanakamilisha safari yao ya elimu na kuleta mchango chanya kwenye familia, jamii, taifa na dunia kwa ujumla”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...