Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE

DIWANI wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikila amepongezwa kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika Soko la Hamvu.

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvu jijini Dodoma.

Iddy alisema “tunaendelea kumshukuru Diwani Bakari Fundikila kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika Soko la Hamvu, tayari ametufahamisha kuwa kiasi cha shilingi 20,000,000 zipo tayari katika akaunti ya kata kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo. Jitihada zote hizo anazifanya kwa kushirikiana na Mheshimiwa Athony Mavunde ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini.

Huyu ndugu yetu Mbunge lazima tumwangalie kwa macho yote mawili kwasababu amejitoa katika kada zote ikiwemo elimu, michezo, afya na maendeleo. Sasa, maendeleo yote haya yatafanyika ikiwa tutawaunga mkono. Ndugu zangu twendeni tukashirikiane. Chama Cha Mapinduzi kinataka kukuza maendeleo katika maeneo yake, lakini sisi wananchi na wanachama tuwe tayari kuunga mkono”.

Nasrat Mussa mkazi wa Hamvu alisema kuwa ujenzi wa Soko la Hamvu utaongeza wigo kwa wananchi kufanya biashara zao sehemu rasmi tofauti na wanavyofanya sasa. 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...