Na Yeremias Ngerangera...Namtumbo.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Ngw'aniduhu Malenya amesema wilaya ya Namtumbo inatarajia kufanya tamasha la siku mbili lililopewa jina la Namtumbo Kihenge.
Malenya alidai Lengo la tamasha Hilo ni kutangaza fursa za uwekezaji kwenye maeneo ya kilimo,madini pamoja na kuhamasisha watalii kuja kutembelea Namtumbo.
Aidha Malenya alifafanua kuwa tamasha Hilo litakuwa la siku mbili Kwa kuwakutanisha watu mbalimbali Ili waweze kuitambua Namtumbo pamoja na fursa zake zilizomo.
Mratibu wa tamasha Hilo ni afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Perez Kamugisha alisema tamasha Hilo limepewa jina la Namtumbo Kihenge Kumaanisha mchango wa wilaya ya Namtumbo katika ghala la hifadhi ya chakula la taifa.
Kamugisha alifafanua kuwa Mkoa wa Ruvuma unaongoza kitaifa katika kuzalisha mazao ya chakula huku wilaya ya Namtumbo ikiongoza katika kuzalisha katika Mkoa wa Ruvuma na kufanya wilaya ya Namtumbo kuchangia katika hifadhi ya chakula katika ghala la taifa.
Hata hivyo Kamugisha alidai Kihenge ni ghala lililotengenezwa Kwa kutumia mianzi na kusiribwa udongo kisha kutumiwa na wakulima kuhifadhia mazao Kwa ajili ya kuweka akiba ya chakula.
Pamoja na hayo Kamugisha alibainisha mambo yatakayofanyika katika tamasha Hilo ni pamoja na kuendesha baiskeli za milimani ,kutakuwa na marathon iliyopewa jina la Namtumbo Kihenge Marathon pamoja na kuwa na mkutano na wadau mbalimbali wa biashara za kilimo,madini na kuwavutia watu mbalimbali kuja kufanya utalii wilayani Namtumbo kutokana na kuwepo Kwa geti la utalii la mwalimu Nyerere pamoja na kumsaidia Mheshimiwa Raisi kutangaza utalii kupitia video vya Royal toure.
Zuberi kosa ni mjumbe wa kamati ya hamasa katika tamasha Hilo alisema maandalizi ya kukagua njia zitakazotumiwa na wakimbiaji wakati wa tamasha Hilo umekamilika.
Kosa alidai wakimbiaji wakati wa tamasha Hilo watakimbia mbio za kilometa 2, kilometa 5 pamoja na kilometa 10 huku maandalizi ya barabara Kwa ajili ya mbio hizo yamekamilika.
Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo la Namtumbo Kihenge anatarajia kuwa waziri wa kilimo mheshimiwa Hussein Mohamed Bashe tarehe 22 na 23 septemba mwaka huu 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...