Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema malengo ya Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora za afya.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo akifungua kituo cha afya Bumbwini Makoba, Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Aidha Rais Dk.Mwinyi alieleza katika hatua za awali zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora kufikia malengo ya kuimarisha miundombinu kwa kujenga hospitali za Wilaya kila Wilaya, hospitali za Mkoa kila Mkoa na hospitali ya Binguni itakayokuwa kubwa zaidi na kutoa huduma za uchunguzi Zanzibar.
Pia hatua nyengine Serikali imeamua kushirikiana na sekta binafsi zitoe huduma katika hospitali za serikali zinazohusisha uchunguzi wa maradhi mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...