NA WILIUM PAUL, MOSHI.

MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Esther Maleko amesema kuwa kwa sasa Serikali inatengeneza utaratibu mzuri wa kutoa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili uweze kuwafikia walengwa.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata ya Mamba kusini Jimbo la Vunjo wilayani Moshi ambapo alisema kuwa Serikali ilikuja kubaini fedha hizo zilikuwa zikitolewa kwa ujanja ujanja bila kufikia wale waliokuwa wakilengwa.

“Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusiana na kunyimwa mikopo hii na wakati mwingine zimekuwa zikitolewa kwa upendeleo ndio maana serikali ikaamua kuzuia kwanza kwa muda ili kutafuta njia nzuri ambayo itatumika ili walengwa wanufaike nazo” alisema Mbunge Ester.

Alisema kuwa, Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi inataka kuona wananchi wote wananufaika bila kuangalia kipato cha mtu na kuwataka kuwa wavumilivu wakati serikali itakapokuja na mpango mzuri wa kukopesha mikopo hiyo isiyo na riba.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...