Na Benny Mwaipaja, Beijing-China.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwiguu Lameck Nchemba, ametoa wito kwa Kampuni ya
Mawasiliano ya Huawei ya China, kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya
kisasa ya teknolojia ya Mawasiliano itakayowezesha nchi kuboresha
ukusanyaji mapato yake ya ndani na kupunguza malalamiko ya watumiaji wa
mifumo hiyo wakiwemo wafanyabiashara.
Dkt. Nchemba ametoa Rai
hiyo Beijing nchini China alipoongoza Ujumbe wa Tanzania kutembelea
Kampuni hiyo Tawi la Beijing ambapo masuala kadhaa ya uwekezaji wa
Kampuni hiyo nchini Tanzania, yalijadiliwa.
Alisema kuwa mifumo
iliyopo nchini ya kukusanya mapato ya ndani ya Serikali haisomani
(haiwasiliani ipasavyo) na kuzua malalamiko kutoka kwa watumiaji lakini
pia hali hiyo inaikosesha Serikali mapato.
Dkt. Nchemba
aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mlipaji Mkuu
wa Serikali Dkt. Natu Elimaamry Mwamba, Balozi wa Tazania nchini China
Mhe. Mbelwa Kairuki na Viongozi wengine wakuu wa Taasisi za Serikali
ikiwemo Tanroads na Shirika la Reli Tanzania TRC, alisema kuwa ujumbe wa
Tanzania umejionea mageuzi makubwa ya Teknolijia ya Habari na
Mawasiliano TEHAM iliyobuniwa na Kampuni hiyo.
Alisema kuwa miaka
michache iliyopita Kampuni hiyo ilikuwa ni ya kawaidia lakini baada ya
kuwekeza kwenye utafiti wa tenolojia janja, Huawei imekuwa Kamouni kubwa
na inayoheshimika ulimwenguni na kwamba inaweza kuisaidia Tanzania
kuboresha mifumo yake ya ukusanyaji mapato yake kwa njia ya kodi
mbalimbali.
Aidha, Dt. Nchemba ameuomba uongozi wa Kampuni hiyo
ambao uliongozwa na Makamu wake wa Rais Bw. Zhang kwenye mazungumzo
hayo, kutoa nafasi kwa vijana wa kitanzania za kuongeza ujuzi wa masuala
ya TEHAMA kwa kuwapa nafasi ya kujifunza kwa vitendo kwenye Kampuni
hiyo ili nchi iwe na vijana wabobezi kwenye masuala ya mawasiliani hivo
kukuza ajira na kujiongezea kipato.
Aliiomba pia Kampuni hiyo
kuwekeza nchini Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kutengeneza simu janja
ili wananchi hususan waishio vijijini wapate simu janja kwa bei nafuu na
ziwasaidie katika kazi zao za kujipatia kipato na kwamba soko kubwa la
ndani ya nchi na nchi jirani ni kivutio kikubwa cha uwekezaji huo.
Akizungumza
kwa niaba ya Makamu wa Rais wa HUWAEI Bw, Zhang, Meneja wa Huawei Tawi
la Tanzania Bw. Russel Zhao, alisema kuwa Kampuni yake imepokea mamobi
ya Serikali kupitia kwa Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na kwamba itaangaza
fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania na kuwekeza mitaji na
teknolojia.
Alisema kuwa uhusiano mzuri na wa muda mrefu uliopo
kati ya China na Tanzania unaendelea kuleta hamasa na kwamba Kampuni
hiyo itaangalia uwezekano wa kurejesha Ofsi yake Tanzania kwa hivi sasa
wanafanya shughuli zao nchini Tanzania kutokea nchi Jirani ya Kenya
Waziri
wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na
ujumbe wake wakisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa mambo ya utafiti
na stratejia ya mifumo ya TEHAMA wa Kampuni ya Mawasiliano ya Huawei Bw.
Chu Wantao, namna walivyofanikiwa kufunga mitambo inayozuia madereva
kufanya makosa ya barabarani wanapoendesha vyombo vya usafiri vya moto,
ikiwemo kuongea na simu, ulevi nk. walipotembelea Kampuni ya Huawei,
Tawi la Beijing, China na kujadili masuala ya uwekezaji wa Kampuni hiyo
nchini Tanzania
Waziri
wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na
ujumbe wake wakisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa mambo ya utafiti
na stratejia ya mifumo ya TEHAMA wa kampuni ya Mawasiliano ya Huwaei
Bw. Chu Wantao, namna walivyofanikiwa kujenga mifumo ya kuboresha elimu
kwa kutumia TEHAMA pamoja na matumizi ya nishati jadidifu,
walipotembelea Kampuni ya Huawei, Tawi la Beijing, China na kujadili
masuala ya uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Tanzania
Waziri
wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na
akizungumza jambo wakati akiongoza Ujumbe wa Tanzania walipotembelea na
kufanya mazungumzo ya kiuwekezaji na uongozi wa Kampuni ya Mawasiliano
ya Huawei ya China, alipofanya ziara ya kikazi katika kKampuni hiyo Tawi
la Beijing na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Huawei
Bw. Zhang (Katikati). Aliyevaa nguo nyekundu ni Katibu Mkuu-Wizara ya
Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw.
Masanja Kadogosa na kulia ni Kamishna wa Idara ya Usimaizi wa Deni la
Serikali, Bw. Japhet Justine.Waziri
wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb),
akipokelewa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mawasiliano ya Huawei Bw.
Zhang, Alipoongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea Kampuni hiyo mjini
Beijing, China, na kujadili masuala ya uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini
Tanzania.
Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa
Tanzania-China- Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi Mkuu wa Shirila la
Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala
wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, Kamishna Idara ya
Usimamizi wa Deni la Serikali-Bw. Japhet Justine na Kamishna Msaidizi
Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melkizedeck Mbise
(Picha na Wizara ya Fedha-Beijing)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...