Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma

Msemaji mkuu wa serikali na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Gerson Msigwa ametoa mwito kwa watanzania kuepuka matapeli wa mitandaoni wanaofanya udanganyifu wa kutumia majina ya viongozi kwa madai yakutoa mikopo kwa wananchi .

Msigwa ametoa tahadhali hiyo Agosti 14, 2023 Jijini Dodoma wakati Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi ( NEEV) , Bi. Being’i Issa akitoa taarifa kuhusu utekelezaji na vipaumbele vya baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema “ kuna matapeli wameingia mtandaoni , wiki iliyopita mtu mmoja karusha link mtandaoni pata mkopo wa chapuchapu , Watanzania tusipende short kati mambo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi serikali imewekea utaratibu wake masuala ya ukopeshaji wa namna hiyo utaratibu wake upo uko chini ya ofisi ya waziri mkuu wanasimamia hakuna kitu kinaitwa mikopo ya chapuchapu mtandaoni kwamba unaingia ndani ya dakika moja umeshapewa hela utaratibu uliowekwa wa kupata mikopo unapitia kwenye ngazi za halmashauri ukienda kule halmashauri utapewa utaratibu utaratibu huo utafuatwa, na utaratibu wa kuwawezesha vijana upo ,”

Hata hivyo ameendelea kuwataka waatanzania kutokuingia kwenye jambo lolote bila kujiridhisha kwa viongozi wa Serikali.

“Nataka niseme kitu kimoja Watanzania tuwe makini , serikali imeweka taasisi mbalimbali mpaka ngazi ya chini kabisa wilayani ziko taasisi za serikali kwenye ngazi za kata kuna watendaji wa kata kabla hujaenda kuchukua mkopo wowote jiridhishe hakuna ubaya ukienda kwa mtendaji wa kata , kijiji hao watakusaidia kuliko kwenda kuingia mkataba unakubaliana na watu unapewa mkopo ambao hauwezi kukusaidia kiuchumi,” amesema msigwa .

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Baraza hilo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi ( NEEV) , Bi. Being’i Issa amewataka wanawake kutokuchukua mikopo (Kausha damu) bila kujua matumizi (biashara ) ya mkopo huo.

Amesema watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye mikopo umiza kutokana na ukosefu wa elimu ya mikopo na kushindwa kuelewa dhana ya mikopo.

“Watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye mikopo ya kausha damu kutokana na mikopo hiyo inatolewa kiurahisi na masharti machache, mara nyingi mtu anaenda kwenye mikopo nahana haya ya mkopo, maana mikopo inapelekea watu wanajiua hivyo tusiende kuchukua mkopo kama huna kitu chakufanyika,” amesema Issa.

“Hali iliyoopo sasa hivi nchini huwezi kupata mkopo kama hauna kitu unachokifanya , wakopeshaji yoyote tulionao sasa hivi kuanzia mabenki mpaka mifuko ya uwezeshaji inahitaji uwe nauzoefu wa kitu unachokifanya nauweze kuonyesha historia ya biashara yako kwahiyo mkopeshaji hawezi kutoa pesa yake bila kuhitaji vitu vyote , na hii inapelekea watu wengi kukosa mikopo kwenye taasisi za fedha kwa kukosa vigezo,” amefafaamua Issa.

Mbali na hayo Katibu Bi. Being’i Issa amesema Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 vituo vya uwezeshaji vimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.4 kwa wajasiriamali 4,017 nchini.

“Mafanikio ya Baraza katika mifuko ya uwezeshaji Hadi Machi, 2023 mikopo yenye thamani ya Shilingi trioni 6.1 ilitolewa kwa wajasiriamali 8,650,257 ikiwa wanawake ni 4,747,321 na wanaume 3,902,936,” amesema Issa.

Amesema vipaumbele vya baraza hilo kwa mwaka 2023/2024 ni kuingia makubaliano na shirika la misaada la Marekani USAID katika kuboresha maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara hapa nchini.

Katibu Issa ameendelea kutaja vipaumbele ni pamoja na baraza litatekeleza programu ya kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika manunuzi ya umma kwa kuendesha mafunzo maalum jinsi ya kutumia mifumo mbalimbali ya manunuzi.

“Baraza litaendeleza na kumaliza urasimishaji wa biashara za wanawake na vijana nchi nzima, hii itasaidia wafanyabiashara kupata mikopo na mafunzo ya biashara”, ameeleza Issa.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari -Maelezo na msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akizungumza katika mkutano na wanahabari wakati Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kuhusu masuala ya Uwezeshaji Tanzania na vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2023/2024 leo agosti 14, 2023 katika ukumbi wa idara ya habari-maelezo Leo jijini Dodoma





Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu masuala ya uwezeshaji Tanzania na vipaumbele kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Agosti 14, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...