Kamati ya ushauri wa watumia maji na nishati Energy Utilities Regulatory Authority (EURA CCC), Mkoa wa Shinyanga imefanya Ziara kutembelea Miradi miwili inayotekelezwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) iliyopo kata ya Tinde halmashauri ya Shinyanga Mkoani Humo.
Ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi imefanyika leo Agosti 17,2023.
Akitoa ufafanuzi wa gharama za miradi na wanufaika wa miradi hiyo Kaimu Mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi Mhandisi Uswege Mussa amesema Mradi wa maji Didia umeghalimu Milioni 92 wenye Ujazo wa lita 94,000. wanaotalajia kunufaikani wakazi 9,210. na Mradi wa maji Tinde Taki la Buchama lenye ujazo wa lita Milioni 1,150,000. utawanufaisha wakazi 60,000 lakini kwa hatua za awalli mpaka sasa wananchi 10,129.wa vijiji viwili kijiji cha Jomu na Nyambui wameanza kunufaika na Mradii huo.
Kaimu Mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi Mhandisi Uswege Mussa Akitoa ufafanuzi wa gharama za miradi na wanufaika wa miradi hiyo.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kudely Sokoine amesema ameridhiswa na utekelezaji wa miradi hiyo inayotekelezwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) katika kata hiyo.
''Niwapongeze sana SHUWASA kwa utekelezaji wa miradii hii kwa sababu maji ni Uhai bora mtu alale gizani kuliko kukosa maji kupitia ziara hii tumeona fedha za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani zinaonekana sisi kama kamati tutaenda kuwa Mabalozi wazuri kwa Wananchi kwa sababu tunaweza kuwa tunawalaumu SHUWASA kumbe Sisi watumia Maji ndio hatulipi kwa wakati tukichelewa kulipa tunawapatia Shida hawa Mamlaka kwa sababu na wao wananunua kutoka kwa KASHWASA". Amesema Kuderi.
Naye Muweka hazina wa Kamati ya ushauri wa watumia maji na nishati Joseph Ndatala ameiomba mamlaka kusambaza maji haraka kwa wananchi kwani huduma bora ni haki ya kila Mwananchi.
"Miongoni mwa huduma za msingi na lazima kwa binadamu yeyote ni Maji miradi hii isikamilike tu harafu wananchi wasinufaike na miradi hii tuhakikishe wananchhi wanapata huduma ya maji kwa sabbabu huduma bora ya Maji ni haki ya kila Mwananchi wa Tanzania'' amesema Ndatala.
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Tinde Edward Charles na Mlila Tumaini Bwile wamesukuru kuwepo kwa huduma hiyo kwani hapo awali walikua wananunua dumu moja la maji Tshs 500/= mpaka 1000/= nyakati za kiangazi huku wakiiomba Mamlaka husika kuangalia bei ambapo kwa Unit moja wananunua kwa Tshs 2,500/= hali inayowapa ugumu wananchi wa kipato cha chini kupata huduma. ya maji safi na salama.
Akifafanua kuhusu bei hiyo Mkurugeni Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoani Shinyanga SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola amekili uwepo wa bei kubwa ya maji kwenye maeneeo hayo huku akiwaomba wakazi wa maeneo hayo kuwa watulifu wakati jambo hilo linashughulikiwa.
"Ni kweli kwa maeneo haya ya Tinde kunabei kubwa ya kununnua maji jambo hili tunalifanyia kazi kufika mwezi wa 9 au wa 10 bei zitakuwa zimeshuka. Amesema Katopola.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kudely Sokoine akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mkazi wa kata ya Didia Tumaini Mlila Bwire. akitoa hoja kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoani Shinyanga SHUWASA kuhusu bei ya maji.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)Mhandisi Yusuph Katopola akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maji.
Kaimu Mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi kutoka SHUWASA Mhandisi Uswege Mussa akitoa ufafanuzi wa gharama za miradi na wanufaika wa miradi hiyo.
Picha ya pamoja Wajumbe wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC Mkoani Shinyanga wakiwa na watumishi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga SHUWASA wakiwa katika Tangi la mradi wa maji Didia wilayani Shinyanga, kushoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...