Katika kukabIli na vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na vitendo vya unyanyasanji kwa Wazee Serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imezindua kituo cha huduma kwa mteja (Jamii Call Center) ambapo kituo hicho kitasaidia kupata taarifa, elimu, huduma na ufumbuzi dhidi ya changamoto za huduma mbalimbali.

Akizungumzia katika ufunguzi wa kituo hicho Leo Jijini Dodoma Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema taarifa zitakazopokelewa katika kituo hicho zitafanyiwa kazi Kwa haraka kulingana na ahadi za Wizara na kutoa huduma zilizoainishwa kwenye Mkataba wa huduma kwa mteja.

Dkt Gwajima ameyasema kituo hicho kitasaidia kutoa elimu kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi (Maendeleo) na mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake na Makundi Maalum wakiwemo machinga, bodaboda, mama lishe na babalishe kupitia Taasisi za fedha na serikalini, utaratibu wa kuwasili watoto na malezi ya kambo, mwongozo na utaratibu dhidi ya manusura wa ukatili na unyanyasanji wa kijinsia kwa watoto.

Pia Dkt Gwajima amesema kituo hicho kitasaidia kutoa msaada wa kisheria kwa manusura WA ukatili WA kijinsia na kwa watoto na haki za wanawake na wajane, Utaratibu kwa Wahanga wa Usafirishaji Haramu wa Binadamu.Utaratibu wa kuokoa Watoto wanaoishi mazingira hatarishi na kufanya kazi mitaani na wazee wasiojiweza na familia duni. Ukatili kwa Watoto mitandaoni.

Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto.Ushauri kwa Vijana balehe.Utaratibu wa msaada wa Kisaikolojia katika jamii, Miongozo kuhusu utatuzi wa migogoro ya familia na ndoa.Marekebisho ya tabia na elimu kwa watoto.Utaratibu wa kusajili na kulipia huduma mbalimbali zikiwemo za mitihani, usajili wa makao ya watoto, vituo vya kulelea watoto mchana (day care centres) na Asasi zisizo za Kiserikali.

 Utaratibu wa kusajili wa Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs), ulipaji wa ada mbalimbali na uwasilishaji wa taarifa za robo na za mwaka.Usajili wa kujiunga na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii, malipo ya ada na upatikananji wa matokeo ya mitihani.Taarifa zingine za pongezi, malalamiko, maoni na ushauri kuhusu huduma zinazohusu maendeleo na ustawi wa jamii.

Namba zitakazotumika kupokea taarifa hizo ni 0262 160250 na 0734 986503. Aidha, Watumishi watakaotoa huduma katika kituo hicho wamepatiwa mafunzo ya kutosha ya namna ya kupokea na kuwajibu wateja. Watumishi hao wanaohudumia hapa wanatoka katika kila idara na Vitengo vya Wizara ili kurahisisha utoaji wa majibu na utatuaji wa kero kulingana na Idara na Vitengo.

Aidha Dkt Gwajima ametoa wito kwa namba zilizotolewa kwa Huduma kuwa, zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa ya jamii yenye uhitaji mbalimbali kupatiwa huduma stahiki.

Na amewapongeza Wizara kwa kufungua na kuzindua Kituo hicho ambacho kilikuwa kinasubiriwa kwa hamu kubwa.

Haya hivyo Dkt Gwajima amesema kuanzishwa kwa kituo hicho kutamuondolea mteja usumbufu usio wa lazima wa kusafiri mwendo mrefu na kuingia gharama zisizo za lazima ili kwenda kupata huduma Wizarani ambazo angepata huko aliko na badala yake akipata changamoto zinazohitaji Wizara iingilie kati basi ataweza kupewa ushauri, mwongozo na ikibidi huduma akiwa katika maeneo ya makazi yake akiendelea na shughuli zake za maendeleo.



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akizungumzia na mmoja wa mteja aliyepiga simu katika kituo cha huduma kwa wateja kilichozinduliwa Leo Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...