Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ujio wa msanii nyota maarufu wa filamu nchini China, Jin Dong utaifungulia milango zaidi Zanzibar kwa soko la watalii kutoka China na kuitangaza kimataifa.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu, Zanzibar alipokutana na msanii huyo ambaye yupo Zanzibar kwa ajili ya kutengeneza filamu.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi alimueleza msanii huyo kuwa Zanzibar ina vivutio vingi vya utalii ikiwemo utalii wa fukwe za bahari zenye mchanga mweupe zinazovutia wengi duniani, utalii wa utamaduni , utalii wa Mji Mkongwe,utalii wa michezo, utalii wa visiwa pamoja na wa Mikutano.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amemtembeza katika miongoni mwa vivutio msanii huyo ikiwemo kisiwa cha Mnemba, maeneo ya Mizingani, Forodhani pamoja na Mji mkongwe .

Msanii Jin Dong ni nyota mkubwa China mwenye ushawishi na wafuasi katika mitandao ya kijamii zaidi ya Milioni 15 pia na kazi zake nyingi za filamu alizoigiza nchini humo .















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...