Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Ndg.Awadh Ali Said, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 28/08/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Mhe.Jaji George Joseph Kazi, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 28/08/2023. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. [Picha na Ikulu] 28/08/2023.
Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi pamoja na Mwenyekiti Mhe.Jaji George Joseph Kazi (kulia) na Viongozi wengine kabla ya kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) hafla iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo. [Picha na Ikulu] 28/08/2023.
Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. [Picha na Ikulu] 28/08/2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...