Njombe
Uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe umechukizwa na baadhi ya wataalamu wa halmashauri ya mji wa Njombe kutokana na kushindwa kutekeleza vizuri baadhi ya miradi kwenye kata ya Uwemba na kusababisha migogoro kwa wananchi na viongozi wa kata hiyo.
Ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Njombe Justine Nusulupila akieleza namna baadhi ya wataalamu wa halmashauri hiyo walivyosababisha migoggoro kwa kushindwa kutekeleza vizuri miradi kwenye kata ya Uwemba.
"Na sio muda mrefu naweka watu ndani,maeneo mengine miradi ile ile inaisha Uwemba miradi inagoma,wala sitaki maelezo ninachohitaji mkaitizame Uwemba katika mtizamo ambao mimi nina mashaka na halmashauri yako haiwezekani miradi ya Uwemba ionekane haitulii"Jastine Nusulupila akimuagiza Mwenyekiti wa halmashauri na mkurugenzi.
Awali baadhi ya viongozi wa Uwemba kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo mbele ya kamati ya siasa wilaya ya Njombe wamesema wamekuwa wakitoa ushauri juu ya utekelezaji wa miradi kwenye kata yao lakini wamekuwa wakishindwa kusikilizwa.
"Tumesema hawatusikii ndugu zangu kwenye hili tusioneane haya"amesema Mwananchi
Naye katibu wa Chama hicho Sure Mwasanguti amesema jambo hilo limekuwa likikwamisha maendeleo kwenye kata ya Uwemba hali ambayo inaweza kupelekea mazingira magumu kwa Chama.
"Na tukiendelea kulemba hapa ndio mambo yanaharibika sisi tuna maslahi na kata hii na huyu diwani hapa ni wa CCM anaelewekaje kwa watu"alisema Mwasanguti
Kwa upande wake Mhandisi wa halmashauri ya mji wa Njombe amesema wao hutumia utaratibu uliowekwa na serikali ili kuwapata mafundi kwa ajili ya miradi huku kaimu mkurugenzi wa halmashauri Thadei Luoga akiomba radhi kwa changamoto zilizojitokeza huku wakiahidi kwenda kuzifanyia kazi.
"Ofisi ya mkurugenzi tutaketi kwa pamoja tuapte yote yaliyobainika na mwisho wa siku tutakuja na ufumbuzi ambao hauturudishi nyuma tuombe radhi sana kwa hilo"alisema Luoga

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...