Na Andrew Chale, Zanzibar.
WASANII wa muziki wa Reggae kutoka mataifa tofauti wameweza kufanya kweli katika siku ya kwanza ya msimu wa tano wa tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki wa Reggae Zanzibar linalofanyika Mambo Club ndani ya viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.
Wasanii Wanne akiwemo Mash Marley kutoka Zanzibar alikuwa wa kwanza kufungua msimu huo wa tano ambapo alipagawisha kwa nyimbo zake mbalimbali zilizokonga nyoyo umati uliofurika kushuhudia tamasha hilo, Agosti 11, 2023.
Awali Mash Marley aliwaambia mashabiki zake kuwa kwa sasa amerejeq rasmi katika muziki huo baada ya kukaa nje kwa miaka 8, akiendelea ba shughuli za kutayarisha muziki na kusimamia wasanii wanaochipukia.
Ambapo aliweza kuimba mwenyewe nyimbo kadhaa na baadae alipanda na wasanii wake walioweza kuimba nyimbo kadhaa na kuamsha shangwe.
Msanii wa Pili kupanda jukwaa hilo alikuwa Maveriq Mavo kutoka Afrika Kusini ambapo alipagawisha kwa nyimbo mbalimbali na baadae alifuatiwa na masanii CWyne Nakulala (Uganda) ambapo aliweza kukonga nyoyo kwa nyimbo zake za shangwe za Reggae na mwisho Msanii na mwandaaji wa muziki wa Reggae Afrika na Ulaya, Sugardady aliweza kupagawisha jukwaa hilo pia.
Muziki wa Reggae umekuwa na ukikuwa kila mwaka visiwani hapa ambapo tayari wageni wa mataifa wamekuwa wakiweka ratiba kufika kuhushudia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Said Omary Hamad 'Side Rasta' ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono uwepo wa tamasha hilo huku akiomba wadau waweze kujitokeza kudhamini kwani linaenda kuwa tamasha la mfano Barani Afrika.
"Mwaka huu ni msimu wa tano wa tamasha. Tunashukuru Serikali kuliunga mkono, hivyo tunaendelea kuomba wadau wajitokeze kudhamini ilikuongeza tija ikiwemo kuvutia wageni wengi zaidi.
Tulianza kidogo kidogo na sasa tunaendelea kukua, Taasisi za Serikali na binafsi hii ni fursa kujitokeza kudhamini matamasha haya ilikusaidiana na Serikali katika kukuza uchumi wa bluu." Amesema Side Rasta.
Tamasha hilo la Zanzibar Reggae Festival 2023, linadhaminiwa na Mgahawa unaoelea baharini eneo la Forodhani Unguja wa Dreamers Island, Dreamers Arusha, Conscious Superstar na wengine wengi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...